. Maana ya Kusimamisha
Swala.
Ni kuswali kwa kutekeleza kikamilifu nguzo, sharti zote za swala na kuwa
na unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.
§
Nafasi na
Umuhimu wa Kusimamisha Swala katika Uislamu.
Swala imesisitizwa na ina umuhimu katika Uislamu kwa sababu zifuatazo;
i.
Kusimamisha Swala ni Amri ya Mwenyezi Mungu
(s.w).
Mwenyezi Mungu (s.w) ameamrisha waumini (waislamu) wote wasimamishe swala
zote za faradh na sunnah ipasavyo.
Rejea Qur’an (29:45), (4:103) na (14:31).
ii.
Kusimamisha swala ni nguzo ya Pili ya
Uislamu.
Baada ya shahada mbili, nguzo ya pili na ya msingi mno katika Uislamu ni
kusimamisha swala.
iii.
Swala humtakasa muislamu na mambo machafu na
maovu.
Bila shaka swala ikiswaliwa vilivyo humuepusha mja na mambo machafu na
maovu.
Rejea Qur’an (29:45).
iv.
Swala ni amali ya mwanzo kabisa kuhesabiwa
siku ya Qiyama.
Swala ya muumini ikitengemaa vizuri ndio sababu ya kufaulu kwake Duniani
na Akhera pia.
Rejea Qur’an (23:1-2,9), (87:14-15) na (22:34-35).
v.
Kutosimamisha swala ni sababu ya mtu
kuingizwa motoni.
Hii ni baada ya muislamu Kupuuza swala kwa kutozingatia sharti na nguzo
zake kikamilifu na kukosa unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.
§
Lengo la
Kusimamisha Swala.
Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumkinga mja na mambo machafu na maovu
kwa kutekeleza kikamilifu sharti, nguzo na sunnah za swala pamoja na kuwa na
khushui ndani ya swala kama ifuatavyo;
i.
Swala inamtakasa mja kwa kuzingatia na kutekeleza
sharti zake zote kikamilifu ambazo ni kuwa twahara, sitara (kujisitiri),
kuchunga wakati wa swala na kuelekea Qibla.
ii.
Swala inamtakasa
mja kwa kutekeleza kikamilifu nguzo na sunnah za swala kama
kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w), kusoma Qur’an, kutoa ahadi ya
kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w), kuomba dua na kutekeleza vitendo vyote
vya swala.