Mambo muhimu anayofanyiwa Muislamu (mtu)
anayekaribia kufa.
Mtu
akikaribia kufa huwa hajiwezi kwa lolote lile pamoja na elimu, ujuzi alionao,
hivyo huhitajia kufanyiwa mambo yafuatayo;
i.
Kuogeshwa, kugishwa mswaki na kumpaka mafuta au
manukato kama kuna uwezekano.
ii.
Kumlaza kwa ubavu wa kulia au chali na kumuelekeza
Qibla iwapo kuna uwezekano.
iii.
Kumpa maji ya kunywa.
iv.
Kutamka (kumsomea) – Shahada “Laa ilaha illallaah”
Abu Said na Abu Hurarirah wamesimulia kuwa, Mtume wa Allah amesema: “Wasomeeni watu wenu wanaokaribia kufa; ‘Laailahaillallaah”
Pia Mu’az bin Jabal amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Yule ambaye maneno yake ya mwisho yatakuwa;
“Laailahaillallaah” ataingia peponi.
(Abu
Daud)
Mambo anayofanyiwa mtu
(maiti) mara tu baada ya kufa.
Baada ya mtu kufa inatuwajibikia tuseme: “Innalillah
wainnailaihraaji’una”. Qur’an (2:156). Kisha kumfanyia maiti mambo yafuatayo:
i.
Kwa taratibu kurudishia mdomo wake usiwe wazi kwa
kufunga kwa kitambaa kutoka kidevuni
na kuzungushia kichwani.
ii.
Kufunga macho ya marehemu na huku ukisema;
“Kwa jina la Allah
na kwa kufuata mila ya Mjumbe wa Allah, Ewe Mola wetu mrahisishie mambo yake ya
sasa na msahilishie mambo yake ya baadaye. Na jaalia anayokutanayo yawe bora
kuliko aliyoyaacha.”
iii.
Lainisha viungo vyake (miguu na mikono) kwa kukunja na
kukunjua taratibu.
- Kama
kuna ugumu maji ya uvuguvugu au mafuta yanaweza kutumika kulaisha na kunyoosha viungo hivyo.
- Baada
ya kulainisha viungo, miguu na mikono inyooshwe na kulazwa uso ukielekezwa Qibla kwenye mkeka au kitanda
kisicho na godoro.
iv.
Maiti avuliwe nguo zote alizokufa nazo na kisha
kufunikwa kwa shuka kubwa
- Ni
vyema afunwe kitambaa tumboni au kuwekewa kitu kizito ili tumbo lisifutuke.
v.
Marashi na ubani vitumike kwa wingi ili kuzima harufu
ya uvundo wa maiti.