Ijumaa, 1 Septemba 2017

NAMA YA KUKABILIANA NA MAFUA.
NAMA YA KUKABILIANA NA MAFUA.
Mafua ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya mafua  na pia inasadikika kuwa zipo takribani aina 200 za virusi hawa wa mafua wakiwemo  rhinoviruses,  parainfluenza viruses, enteroinfluenza viruses na vingine vingi. Virusi hivi hupatikana kwa kukutana na hewa yenye virusi hawa, pindi unapovuta hewa yenye mchanganyiko wa virusi hawa. Sababu zingine zinazosadikika kusababisha mafua ni panoja na sigara, moshi, mavumbi, baridi kuwa kali au kuchafuka kwa hewa.

Udonjwa wa mafua unadalili tofauti tofauti na huenda zikafanana na ugonjwa wa malaria. Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kukosa hamu ya kula, kuhisi uchovu, kutokwa na makamasi mengi, koo kukereketa, maumivu ya kichwa na kupiga chafya mara kwa mara. Japo dalili za mafua hutofautiona kwa mtu na mtu kulingana na uwezo wa mwili wake kupambana na magonjwa ila hizi dalili tulizozitaja huwa maarufu kwa watu wengi.

Mgonjwa wa mafua huenda akawa amechoka sana kiasi kwamba analala kitandani kwa homa kali aliyo nayo. Mafua huwaathiri zaidi watoto na wazee kwani miili yao haina kinga za kutosha kupambana na maradhi. Kwa wale wenye HIV+ ugonjwa wa mafua pia hueza ukawaletea athari kubwa sana ikiwemo homa kali na uchovu.

Mtu ana weza kujikinga na mafua kwa kuosha mikono kabla na baada ya kula,  kuziba mdomo anapopiga chafya. Kula vyakula vyenye vitamin A na C kwa wingi, kunywa maji mengi na kupunguza mawazo yaani ”stress”  kwa lunga ya kigeni hapa kinacho maanishwa ni kuwa na furaha. Jambo la msingi limgine ni kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mare humuepusha mtu na mafua kwa kiasi kikubwa.
Miongoni mwa vyakula anavyotakiwa ale mwenye mafua ni kama mboga za majani  zenye vitanimi kwa wingi, kwa mfano spinach, na mchicha. Pia kula matunda yenye vitamin C kwa wingi kama mapapai, na machungwa. Vyakula hivi husaidia katika kuupa mwili uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi na mashambulizi mengine. Maji ya kutosha humsaidia mtu mwili wake kuweza kufanya kazi ya kudhibiti maambukizi kwa urahisi. Hali kadhalika kufaya mazoezi husaidia mwili kufanya kazi vizuri. Pia anashauriwa mgomjwa wa mafua awe chai.

Wapo baadhi ya wataalamu wa tiba mbadala wanazungumzia matumizi ya kitunguu maji kuhusu kutibu mafua. Wanatumia harufu ya kitunguu maji kutibu mafua. Mgonjwa atachukuwa kitunguu kasha ataondowa majani, au maganda ya juu kisha atakuwa anavuta haruvu ya kitungu. Atafanya hivyo kwa mara kadhaa hasa anapokwenda kulala.