Kansa ni katika magonjwa yanayosumbuwa kwa
kiasi kikubwa leo duniani. Kansa huweza kusababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo uvutaji wa sigara kwa 31%,
vyakula kwa 37%, pombe kwa 3% na nyingine nyingi. Katika sababu hizi vyakula
huchukuwa nafasi kubwa katika kusababisha kansa.
Mwaka 2015 watu milioni 90.5 waligungulika
kuwa na kansa. Inakadiriwa kuwa kila mwaka takribani watu milioni 14.1
wanaupata kansa kila mwaka. Watu milioni 15.7 walikufa na kansa ambayo ni sawa
na asilimia 15.7% ya vifo vyote mwaka huo.
CHATI INAYOONESHA SABABU ZA
KANSA (CANCER)
1.
VITUNGUU THAUMU ( GARLIC)
Hivi vina kiasi kikubwa cha madini ya salfa
(sulphur compounds) ambayo husaidia kuimarisha mfumo wa afya mwilini (immune
system) Pia wanasayansi wanafahamu kuwa
kitunguu thaumu kinasaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya tumbo.
2.
Samaki
Tafiti za kisayansi zilizofanyika Australia zimegunduwa kuwa ulaji wa samaki mara 4 au zaidi humuepusha
mtu na kansa ya damu ( blood cancers leukemia, myekoma, and non- Hodgkin’s
lymphoma). Samaki wanaoshauriwa zaidi ni wale wenye mafuta kwa wingi kama
salmon.
3.
Apple (maepo)
Matunda haya yanafahamika kwa uwezo wake
mkubwa wa kuuwa seli za kansa. Tafiti za kisayansi zilizofanywa nchini Ujerumani
zinathibitisha uwepo wa procyanidins ambayo hufahamika kudhibiti seli za kansa
kutengenezwa ndani ya mwili.
4.
Avocado (palachichi)
Matunda haya pia husaidia kwa kiwango kikubwa kupambana na
seli za kansa. Fat iliyoko kwenye matunda haya huweza kusaidia kwa iwango
kikubwa kupambana na kansa.
5.
Kabichi ( cabbage)
Kabichi hujulikana kwa kuwa na bioflavonoids
kemikali ambazo hupambana na seli za kansa. Kabichi kusaidia kupambana na kansa
ya tumbo kansa ya matiti na aina zingine za kansa.
6.
Karoti ( carrots)
Karoti zina alpha-carotene na
bioflavonoids ambazo husaidia katika kupambana na seli za kansa. Karoti huweza
kupambana hasa na kansa ya ini. Wanasayansi pia wanatahadharisha matumizi ya
karoti kwa kiasi kikubwa kwa mtu anayevuta sigara.
7. 7.Tende
Tende hujulikana kuwa na polyphenols ambazo
husaidia kupambana na kansa kwa kiwango kikubwa. Vitamin B12 na fiber katika
tende husaidi kwa kuiwango kupambana na aina mbalimbali za kansa.
8. Mayai yana
vitamin D kwa kiwango kukubwa. Vitamin hivi pia hufahamika kwa uwezo wake wa
kupambana na seli za kansa.
9. Tangawizi
10. Komamanga
11. njegere
Tungependa kutoa ushauri kwa dada na ndugu
hao ambao huvuta na kunywa pombe kwamba haya yote yana kemikali ambazo
zinajulikana kwa kuwa na uwezo wa kusababisha kansa. Kwa hivyo wanapaswa
kuchukua maandalizi kabla hali inakuwa mbaya zaidi katika afya yao.