Jumapili, 22 Oktoba 2017

HIVI NDIO VYAKULA UNAVYOTAKIWA KULA

                         
Chakula bora ni muhimu kwa afya yako. Ulaji mzuri wa chakula unaweza kukuondoshea madhara na hatari za baadhi ya magonjwa. Ulaji mzuri wa chakula utaweza  kuupa mwili wako kunga ya kupambana dhidi ya maradhi na mashambulizi mengine. Halikadhalika ulambaya wa chakula unaweza kuleta hatari ndani ya mwili wako kama vile magonjwa ya kisukari na saratani.

Mtu anatakuwa kuala chakula bora na si chakula chochote kile. Mlo kamili huzingatiwa pale mtu anapokula mlo ambao una ndani yake virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini. Virutubisho hivi ni maji, protini, fat na mafuta pamoja na madini. Virutubisho hivi vinafanya kazi mbalimbali ndani ya mwili zikiwemo kulinda mwili, kujenga na kukarabati mwili pamoja na kuutibu mwili.

             Vyakula vya protini

Hivi ni vyakula ambavyo vinakazi ya kuujenga mwili pamoja na kuukarabati mwili. Kupona kwa vidonda na makovu vyote ni kazi ya protini. Uotaji wa nywele mpya pamoja na kukuwa kwa kucha baada ya kuzikata vyoye hivi hufanyika shukrani kwa vyakula vya protini.

Unaweza kuvipata vyakula vya protini kutokana na maziwa, nyama, mayai, na samaki. Katika mimea pia unaweza kupata protini kwa kula maharage, mchele na baadhi ya nafaka zingine. Pia ulaji wa mboga za majani unaweza kusaidia kupatikana kwa protini.

             Vyakula vya fat na mafuta

Vyakula vya fati husaidia katika kuupa mwili nguvu. Fat husaidia kulinda seli zilizomo mwilini zisizurike. Vyakula hivi huupa mwili joto hususan wakati wa baridi. Na inashauriwa wakati wa baridi kula vyakula vya fat kwa wingi ili kuupa mwili joto. Vyakula vya fat pia husaidia kuganda kwa damu pindi mtu anapopata jeraha.
Vyakula vya fati ni maziwa, mafuta ya wanyama, mayai na nyama. Pia katika matunda fat inapatikana kwa wingi pia kwa mfano katika avocardo, olive, karanga , alizeyi pamoja na mafuta ya mimea yaani vegetable oil. Samaki ni chanzo kizuri cha fat.

            Vyakuala vya vitamin na madini

Mwili unahitaji vyakula hivi ili uwezesj\he matumizi ya vyakula vingine yawe mazuri tunahitaji viyamini kwa kuulinda mwili dhidi ya magonkwa. Vitamin c hujulikana kwa kusaidia ugonjwa wa scuvy ugonjwa huu humfanya mtu atoke samu mwenue mafinzi. Vitamin A husaidia kurekebisha afya ya macho. Vitamin K husaidia kuganda kwa damu unapopata jeraha.
Mwili unahitaji madini pia ili uweze kujikinga na hatari zingine. Madini ya chuma ni muhimu katika kujenga seli nyekundu za damu.madini ya calcium ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno
Madini na vitamin hpatikana zaidi kwenye mboga za majani,  na matunda. Matunda yenye uchachu kama limao, chungwa husaidia kwa vitamin C na mapapai pi hujulukana kwa kuwa na vitamin C. spinachi ni muhimu kwa vitamin A. samaki husaidia kwa madini menhine.

                       Vyakula vya wanga

Vyakula vya wanga ndio vyanzo vikuu vya nguvu ndani ya mwili. Vyakula hivi hupatikana kwenye starch. Mwili unatumia vyakula vya wanga katika hali ya glucose. Ambayo huenda maeneo mengine ya mwili kwa ajili ya kuzalisha energy.
Unawza kupata wanga kwa kula nafaka kama maharage, matama, mihogo. Pia asali, miwa na viazi ni vyanzo vizuri vya wanga.

                Maji

Zaidi ya 70% ya mwili wa binadamu ni maji. Tunahiyaji maji ili tuweze kuishi. Mmaji ni muhimu kwa afya. Mtu anahitaji kunywa maji bilauri  8 mpaka 10 za maji. Mtu anaweza kuishi siku ziaizopungua 8bila kunya maji lakini anaweza siku nyingi zaidi bila ya kutokula chakula.
Maji husaidia kurekebisha mifumo mbalimbali ndani ya mwili kama vile mfumo wa utoaji takamwili, mfumo wa chakula na mfumo wa damu. Maji husaidia katika kutibu maumivu ya kichwa amabayo yamesababishwa na unywaji mchache wa maji.

       VYAKULA VYA KAMBAKAMBA
Hii si katika aina vya virutubisho. Hivi ni vyakula ambavyo husaidia katika msukumo wa chakula tumboni. Husaidia katika kufanya haja kubwa itoke kwa usalama. Matatizo ya kuziba kwa choo au kupata hajakubwa kwa kiasi kidogo husababishwa na kutokula vyakula vyenye hali hii kwa kiwango kinacho hitajika.

Tunaweza kupata roughage kwenye nafaka zote zisizo kobolewa, matunda, maharage, kabichi spinach, mihogo na nyanya sikisizo menya na jamii zingine za vyakula hivi.