Umuhimu na Msisitizo wa Zakat na Sadakat katika Uislamu.
i.Zakat ni nguzo ya tatu ya Uislamu.
ii.Kutoa zakat na Sadaka ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (14:31) na (2:254).
iii.Kutoa Zakat ndio kitambulisho cha Uislamu na Ucha-Mungu wa mtu.
Rejea Qur’an (9:11) na (2:2-3).
iv.Kutoa Zakat na sadaka ni sababu ya mtu kufaulu Duniani na Akhera.
Rejea Qur’an (2:2-3), (23:1-4), (22:34-45) na (2:262,274).
v.Kutotoa Zakat na Sadaka ni sababu ya kuangamia mtu Duniani na Akhera.
Rejea Qur’an (9:34-35), (92:8-10) na (3:180).
§Masharti ya Utoaji wa Zakat na Sadaqat.
(a)Kutoa vilivyo halali.
(b)Kutoa vilivyo vizuri.
(c)Kutoa kwa kati na kati.
(d)Kuwapa wanaostahiki.
(e)Kujiepusha na ria na kufuatilia kwa masimbulizi.
(a)Kutoa Vilivyo halali.
- Mali ya halali na iliyochumwa kwa njia ya halali ndio inayofaa kutolewa Zakat ua Sadaqat. Mali ya haramu au iliyochumwa kwa njia ya haramu haikubaliki.
Rejea Qur’an (4:10), (23:51) na (2:172).
(b)Kutoa Vilivyo vizuri.
- Ni kutoa kile ukipendacho kwa dhati na ndio zina malipo makubwa kwa Allah.
Rejea Qur’an (2:267) na (3:92).
(c)Kutoa kwa kati na kati.
- Ni kutoa kwa kuzingatia kipimo (kiasi) ambacho hakiwezi kukuathiri katika matumizi ya maisha yako na familia pia.
Rejea Qur’an (2:219) na (17:29).
(d)Kujiepusha na ria na masimbulizi.
- Ni kutoa mali au huduma kwa ajili ya Allah pasina kujionyesha na kufuatilia kwa masimbulizi.
Rejea Qur’an (2:264), (2:271) na (2:274).
(e)Kuwapa Wanaostahiki.
- Zakat au Sadaqat hutolewa kupewa watu maalumu wanaohitajia, wenye matatizo na zikitolewa kwa asiyestahiki, huwa ni dhuluma.
Rejea Qur’an (9:60).
§Wanaostahiki kupewa Zakat.
Kwa mujibu wa Qur’an (9:60) na (2:273), wanaostahiki kupewa Zakat ni waislamu tu katika makundi yafuatayo;
i.Fukara.
- Ni kundi la wale wasiojiweza kwa chochote cha kumudu maisha yao kabisa ya kila siku bila kusaidiwa.
ii.Maskini.
- Ni wale wasio na uwezo wa kupata mahitaji yao ya msingi ya kimaisha ila wana uwezo wa kujikimu kwa kiasi fulani tu.
iii.Wanaozitumikia (Al-A’miliina A’laihaa).
- Ni wale wote wanaozikusanya na kuzigawanya kwa wanaohusika bila kujali uwezo wao.
iv.Wanaotiwa nguvu nyoyo zao juu ya Uislamu.
- Ni wale walioingia katika Uislamu karibuni na wanahitajika kuimarishwa imani zao juu ya Uislamu.
v.Kuwakomboa Watumwa (Fir-riqaabu).
- Ni kuwakomboa au kuwanunua watumwa au watu wote wanaoishi chini ya miliki ya watu (mabwana) na kuwaachia huru.
vi.Kuwasaidia wanaodaiwa kulipa madeni yao.
- Ni kuwalipia waislamu madeni yao waliokopa ili kujikimu kimaisha lakini bila kukusudia wameshindwa kulipa deni zao.
vii.Kutumika Katika njia ya Allah (s.w).
- Ni kutumika katika shughuli zote zinazopelekea kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii.
viii.Kuwasaidia Wasafiri walioharibikiwa njiani (Ibnis-sabiil).
- Msafiri yeyote muislamu aliyeharibikiwa kwa kupoteza, kuibiwa au kuishiwa mali yake hata kama ni tajiri, ni wajibu kupewa zakat.
§Wanaostahiki kupewa Sadaqat.
Kwa mujibu wa Qur’an (4:36) na (51:9);
- Sadaqat hupewa wale wale wanaopewa Zakat lakini bila kiwango au muda
maalumu au kufikia nisaab.
- Sadaqat hupewa mwanaadamu yeyote hata wasiokuwa Waislamu ikiwa tu ni
mwenye kuhitajia.
- Kila muislamu anao uwezo wa kutoa sadaqat, kwani inahusika na kutoa mali,
huduma, tabia nzuri, n.k.
Rejea Qur’an (2:263).
- Pia haifai kurejesha sadaqat baada ya kuitoa.
>>> Bofya hapa kupata yanayojiri katika blog hii
>>> Bofya hapa kuungana nasi youtube ili upate video zetu nyingine
>>> Bofya hapa kupata masomo zaidi ya afya ukiwa na app yetu
>>> Ungana nami kwenye FACEBOOK