Ijumaa, 27 Aprili 2018

MTAJE ALLAH KWA JINA HILI, DUA YAKO ITAKUBALIWA.

                                       
   
                           UTANGULIZI
Sifa njema zinamstahikia Allah Mola wa ulimwengu. Rehma na amani zimshukie mtume wa Allah (s.a.w). Ama baada ya utangulizi huu mfupi, huu ni mwendelezo wa darsa za dua. Hapa utajifunza kuhusu watu ambao dua zao ni zenye kukubaliwa. Pamoja na kutekeleza taratibu zote za dua ila kuna watu ambao wakiomba dua zao huwa hazirudi.

Unaweza kupata darsa zote za dua kupitia simu yako ya kiganja. ingia play store kisha andika darsa za dua. au >>bofya hapa>> kudowanload App usome dua mbalimbali.
Tumeona katika darsa zilizopita kuhusu adabu za kuomba dua bofya hapa kusoma pamoja na fadhi la za dua bofya hapa kusoma na mengine. leo tutaona nyakati ambazo ni mahususi kuomba dua.

                                  JINA KUBWA LA ALLAH
Kuomba dua kwa kutumia jina la Allah lililo kubwa. Allah ana majina mengi na mazuri. Lakini katika majina hayo lipo ambalo ni kubwa na ukiomba dua kwalo lakina utajibiwa. Kwa ufupi ni kuwa jina hili limefichwa na hakina yeyote anayelijuwa. Ila mtume ametowa ishara ya kuonesha wapi linapatikana na maneno gani mtu atumie kulipata jina hilo. Amesema mtume صلّي الله عليه وسلّم “jina kubwa la Allah lipo kwenye aya sita za mwisho za surat hashri. (amepokea Dilamy kutoka kwa Ibn ‘Abas). Pia katika mapokezi mengine ya Tabrany kutoka kwa Ibn ‘Abas kuwa mtume amesema jina kubwa lipo kwenye aya ya 20 ya surat al-imran. Na pia zipo hadithi nyingi sana zinazoashiri wapi jina hilo lipo. Nitaleta chache tuu.

  i) Aisha رضىالله عنها aliomba dua hiiALLAHUMMA INII AD’UKA LLAHA WA-AD’UKAR-RAHMANA, WA-AD’UKAL-BARRAR-RAHIIMA, WA-AD’UKA BIASMAAIKAL-HUSNAA KULLIHAA MAA ‘ALIMTU WAMAA LAM A’ALAM AN TAGHFIRA LII WATARHAMNII” Mtume akacheka kisha akasema “hakika jina kubwa lipo ndani ya dua hii. (amepokea Ibn Maajah kutoka kwa ‘Aisha) hadithi hii ni ndefu nimeikatisha na kuchukua hiyo dyua tu.
  ii)hadithi ya Anasرضىالله عنهkuwa”
 عَنْ أَنَسٍ، قَالَ دَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم الْمَسْجِدَ وَرَجُلٌ قَدْ صَلَّى وَهُوَ يَدْعُو وَيَقُولُ فِي دُعَائِهِ اللَّهُمَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ الْمَنَّانُ بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ ذَا الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ ‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ تَدْرُونَ بِمَ دَعَا اللَّهَ دَعَا اللَّهَ بِاسْمِهِ الأَعْظَمِ الَّذِي إِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ وَإِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى ‏

"amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa alikuwa amekaa na mtume صلّي الله عليه وسلّم wamekaa msikitini na kulikuwa na mtu mmoja anaswali kisha akaomba dua kwa kusema “ ALLAHUMMA ANNII AS-ALUKA BIANNALAKAL-HAMDA, LAA ILAAHA ILLA ANTAL-MANNAANU BADI’US-SAMAAWATI WAL-ARDH YAA DHALJALALI WAL-IKRAM YAA HAYYU YAA QAYYUUM” akasema Mtume صلّي الله عليه وسلّم umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo anapoombwa kwalo atajibu”. (amepokea tirmidh kwa isnad gharib).




soma hadithi
za ALIF LELA
bofya hapa
  




 Iii)amesimulia Abdillah Ibn Buraydah رضىالله عنه kutoka kwa baba yake kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم alimsikia mtu mmoja akisema “ALLAHUMMA INNIASALUKA BIAN-ASHHADU ANNAKA ANTALLAHU LAA ILAAHA ILLA ANTA. AL-AHADUS-SWAMADUL-LADHII LAMYALID WALAM YUULAD, WALAM YAKUN LAHU KUFWAN AHAD” akasema Mtume صلّي الله عليه وسلّم hakika umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo akiombwa hutoa na akiombwa dua hujibu. (amesimulia Abuu Daud,tirmidh,Ibn Maajah na Ibn Hiban).
  Iv). Mtume amesema katika mapokezi mengine kuwa
 اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ فِي هَاتَيْنِ الآيَتَيْنِ ‏{وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ}‏ وَفَاتِحَةِ سُورَةِ آلِ عِمْرَانَ ‏"
Jina kubwa la Allah linapatikana kwenye aya hizi‘ waillahukum ilahu wahidu laa ilaaha illa huwar-rahmanir-rahiim’ na mwanzoni mwa surat al ‘Imran .

Kwa ufupi ni kuwa jhina hili hakuna anayelijuwa ila wachacehe katika wale ambao Allah amewachaguwa. Ila Mtume (s.a.w) ametaja ishara za kulipata jina hili. Hivyo kupitia ishara hizo mwenye kuomba dua anawezakulitumia jina hili. Allah ndiye anajuwa zaidi juu ya jambo hili.

Unaweza kusoma darsa zote za dua katika simu yako ya kignja bofya hapa. In Shaa Allah panapo majaaliwa tutawaletea darsa za qurani pamoja na tajweed. tunanamuomba Allah atupe wepesi juu ya hili. pia tunathamini mchango wenu ndugu wasomaji pindi utakapoona kosa lolote katika darsa zetu tunaomba utuelekeze ama kama una jambo unataka kuchangia tafadhali wasiliana nasi kwa namba +255712939055 kama hautatupata tutumie sma kwa nmba hiyohiyo au barua pepe rajabumahe@gmail.com.


UHIMU KWA AJILI YAKO
Jifunze zaidi kuhusu Afya yako na lishe ukiwa na program zetu kwenye simu yako ya kiganja. bofya link zifua tazo kupata elimu zaidi juu ya afya yako
1.Afya na lishe bofya hapa
2.afya yako. bofya hapa
3.kupata post zetu moja kwa moja . bofya hapa



NYINGINEZO