Alhamisi, 27 Septemba 2018

Maana y swala


Maana ya Swala
 Maana ya Swala kilugha
(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua. Katika Qur-an tunaamrishwa kumswalia Mtume, yaani kumuombea dua Mtume (s.a.w) katika aya ifuatayo: Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Mtume (wanamtakia Rehema). Basi, enyi mlioamini mswalieni (muombeeni au mtakieni Mtume) Rehema na muombeeni amani (33:56)


Vile vile katika Hadith, Mtume (s.a.w) anatuambia: Yule atakayealikwa kwenye karamu ya harusi aitikie wito huo, kama hataweza kuitika amswalie (amuombee dua) aliyemkaribisha. (Muslimu).

Maana ya swala Kisheria:
(b) Kisheria Katika sheria ya Kiislamu, swalaa ni maombi maalumu kwa Allah (s.w) yanayofanywa kwa kufuata utaratibu maalumu uliowekwa na Allah (s.w) na kufundishwa kwa matendo na Mtume wake. Katika maombi haya maalumu mwili mzima huhusika katika maombi haya kwa kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, kukaa na kuzingatia yale yote anayosema katika kuleta maombi haya.