Alhamisi, 26 Desemba 2019

ONGEZA USALAMA WA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK

ONGEZA USALAMA WA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK  (Two-Factor Authentication).

Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Akaunti kuhakiwa inamaana kuna mtu amelogin kwenye akaunti yako bila ya ruhusa yako ama bila ya kumpatia neno la siri. Facebook imeweka njia kadhaa kuhakikisha kuwa akaunti za watu zipo salama muda wowote.



Two-factor authentication ni katika njia mujarabu ambazo facebook wameweka ili kulinda akaunti za watumiaji wake. Kwa kutumia njia hii hata kama mtu anaijuwa password yako (neno la siri) hataweza kuingia kwenye akaunti yako ya facebook mpaka awe na laini yako ambayo namba yeke umeisajili facebook.



Njia hii inaongeza tabaka lingine la usalama wa akaunti yako ya facebook. Baada ya kuingiza neno la siri kwenye akaunti yako ya facebook, facebook watakutumia code (namba sita) kwenye laini yako ulioisajili facebook. Namba hizo utaziingiza kwenye kibox na ndipo utaruhusiwa kuingia kwenye akaunti.



Kuanza kutumia  njia hii ingia kwenye setting, kisha security and login kisha Two-Factor Authentication. Utatakiwa kuingiza namba ya simu na maelekezo machache yatafuata. Utalogout kisha utalogin tena ili kuthibitisha huduma kama ipo tayari.

Wasiliana nami kwa maelezo zaidi, au nofya link hapo chini.
Endelea