Jumapili, 22 Machi 2020

VITAMINI K NA FAIDA ZAKE MWILINI


Vitamini ni virutubisho ambavyo mwili unavihitajia katika kuhakikisha michakato mbalimbali ndani ya mwili inafanyika. Vitamini vipo katika makundi mengi kama vitamini A, B, C, D na K. Kila kundi kati ya hivi linaweza kugawanyika katika vikundi vijidogo. Kwa mfano vitamini B vinaweza kuwa B1, B3, B6 na B12. kila mmoja kati ya vitamini huwa na kazi yake maalumu. Na upungufu wowote wa vitamini hivi unaweza kusababisha madhara kwenye afya ya mtu.


Katika makala hii tutakwenda kuona vitamini K kwa kuangalia makundi yake, kazi zake, wapi tunaweza kuvipata na ni zipi athari za kuvikosa vitamini hivi kwenye miili yetu. Makala hii kwa kirefu zaidi unaweza kuipata kweye tovuti yetu, bofya link hii hapa.

Vitamini K mwa mara ya kwanza vimetambulishwa na mwanasayansi kutokea Danish aliyetambulika kwa jina la Henrik Dam mwaka 1929. baada ya hapo tafiti mbalimbali zikafanyika. Vitamini hivi vimegawanyika katika K1 na K2. kazi nyingi za vitamini K huweza kuafya zaidi na kundi hili la vitamini K1. vitamini K1 unaweza kuvipata kwenye mbog za majani za rangi ya kijani na K2 unaweza kuvipata kwenye nyama, na mayai.

Tunawza kupata vitamini K kwa kula vuakila kama;
1. Mboga za majani za rangi ya kijani kama kabichi, mchicha na spinach
2. Mayai
3. Nyama
4. Maziwa
5. Mapalachichi
6. Zabibu

Kama ilivyovitamini vingine basi vitamini K vina kazi mbalimbali mwilini. Kazi kubwa ya vitamini K ni kuhakikisha damu inaganda badala ya kupata jeraha. Yaani pindi ukijikata ama kuchubuka damu inatoka, hivyo vitamini K vitasaidia kuhakikisha kuwa damu inakata. Pia kuzuia damu isitoke kwenye maeneo mengine ya mwili kama mdomoni.

Wataalamu wa afya wanahusisha pia vitamini K na uboreshwaji wa afya ya ubongo, moyo na mifupa. Vitamini K husaidia katika kuboresha utunzaji wa kumbukumbu hasa kwa wale wenye tatizo la kusahausahau. Husaidia kuimarisha afya ya mifupa na kuifanya iwe imara na isiyopasuka kwa urahisi. Huepusha na maradhi ya mifupa yaitwayo osteoporosis. hupunguza uwezekano wa kuganda kwa madini ya calcium kwenye mirija ya damu na kuboresha msukumo wa damu.

Kama tulivyoziona kazi za vitamini K basi upungufu wa vitamini hivi unaweza kusababisha damu kutoka kwa muda mrefu kwenye majeraha bila kukata. Pia damu inaweza kutoka hata kama huna majeraha kwenye pua ama mdomo.

Upungufu wa vitamini K pia unaweza kuhatarisha afya ya moyo, mifupa na uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu. Mwenye upungufu wa vitamini K anaweza kupata saratani kwa urahisi,pia maradhi ya moyo anaweza kuyapata hususan shinikizo la juu la damu.

Makala nyingine kwa ajili yko
Makala hizi na nyinginezo unaweza kuzipata kwenye tovuti yetu. Pia unaweza kusoma:-
Afya ya uzazi
Darasa za matunda na Afya
Darasa la afya
Afya na maradhi
Afya na lishe