Alhamisi, 26 Machi 2020

VYAKULA VYA VITAMINI C, JE NI ZIPI KAZI ZA VITAMINI C NA DALILI ZA UPUNGUFU WA VITAMINI C



VYAKULA VYA VITAMINI C, JE NI ZIPI KAZI ZA VITAMINI C NA DALILI ZA UPUNGUFU WA VITAMINI C

Vitamini C ni vitamini ambayo hufahamika kama ascobic acid ama ascorbate. Imeitwa vitamini C kwa sababu ascobic acid huwakilishwa na alama C. vitamini C imekundulika miaka ya 1920. vitamini hii husaidia kuilinda miili yetu dhidi ya ugonjwa wa kiseyeye yaani scurvy.



Vitamini C tunaweza kuvipata katika matunda yenye uchachu kama machungwa, maembe, ndimu, limao, machenzza na mengineyo. Pia tunaweza kupata vitamini C kwenye matunda ya rangi a njano kama nanasi, embe, pera, papai na pensheni. Pia katka matunda kama mapalachicchi nyanya, pilipili, tunguja. Pia katika mayai, maini na maziwa.


Upungufu wa vitamini C unaweza kusababisha kupata maradhi ya kiseyeye. maradhi haya yanaweza kupelekea damu kutoka kwenye mafinzi, maumivu ya misuli, viungio na mifupa, kushindwa kupumua vyema na mwili kukosa nguvu. Ugonjwa huu pia unaweza kupelekea kifo. Pia upingufu wa vitamini C uanaweza kusababisha kuchelewa kupona kwa vidonda.


Pia vitamini C vinasaidia kulinda miili yetu dhidi ya maradhi, kwa kuupa nguvu mfumo wa kinga, vitamini C husaidia kuuwa seli za saratani. Vitamini C husaidia kulinda na kuimarisha afya ya ubongo, moyo na mishipa ya damu. Vitamini C husaidia miili yetu katika kupambana na sumu za vyakula.

Kusoma maada hii kwa urefu bofya hapa

Makala hizi na nyinginezo unaweza kuzipata kwenye tovuti yetu. Pia unaweza kusoma:-
Afya ya uzazi
Darasa za matunda na Afya
Darasa la afya
Afya na maradhi
Afya na lishe