Jumamosi, 25 Machi 2017

IJUWE MAANA YA SHUFAA NA NANI ANANASTAHIKI KUPATA SHUFAA (UOMBEZI)

                           Dhana ya Shufaa (uombezi) katika Uislamu.

Maana ya Shufaa kwa mujibu wa Qur’an na Hadith sahihi:
Ni uombezi utakaotolewa na wale walipewa idhini na Allah (s.w) kuwaombea watu watakaokuwa katika udhalili na dhiki katika maisha ya akhera.
Shufaa (uombezi) utakuwa kwa ajili ya;
(i) Watu wafanyiwae hisabu nyepesi
(ii) Watolewe motoni na kupelekwa peponi
(iii) Waingizwe peponi wale ambao mizani ya mema na mabaya yao imekuwa sawa sawa.
(iv) Waja wema waingizwe moja kwa moja peponi bila kuhisabiwa.
(v) Wapandishwe daraja za pepo kutoka daraja ya chini kwenda daraja ya juu.

                          Masharti ya Shufaa (Uombezi)

o Uombezi (shufaa) hautafanyika kwa misingi ya upendeleo wa udugu, urafiki, ukoo, utaifa wa aina yeyote ile.
o Shufaa kwa watu itakuwa kwa idhini ya Allah (s.w) peke yake ili kuombewa watu wa aina mbali mbali.
o Shufaa kwa mja itakubaliwa tu kama alikuwa muumini aliyefanya mema lakini kwa namna moja au nyingine aliteleza na kufanya makosa yaliyo mweka kwenye dhiki.
o Baada ya shufaa (uombezi), ni hiari ya Allah (s.w) kukubali au kukataa uombezi huo.
o Shufaa (uombezi) mwingine utafanyika baada ya mtu (muombewaji) kuadhibiwa motoni kwanza.
o Shufaa haitakubaliwa kamwe kwa makafiri, washirikina na wanafiki hata kama itaombwa na mitume au vipenzi wa Allah (s.w).
Rejea Qur’an (11:42-46), (9:80).


                              Watakaoshufaia (watakao ombea)

Kwa mujibu wa Qur’an na Hadith, watakaoshufaia (watakao ombea) ni;
a) Malaika
b) Mitume
Uk. 20 kati ya 1 3 1
c) Watu wema
d) Watoto waliokufa wakiwa wachanga
e) Amali njema kama swala, funga, zaka, n.k.
f) Qur’an n.k.

                              Watakaoshufaiwa (watakao ombewa)

Kwa mujibu wa Qur’an na Hadith, shufaa itakuwa kwa idhini ya Allah (s.w) kuombewa watu kulingana na matendo yao kama ifuatavyo;
i. Malaika waja (waumini) wema.
ii. Mitume watawashufaia (watawaombea) wafuasi wao waliowafuata kwa uadilifu.
iii. Watu wema watawashufaia jamaa, jirani, rafiki zao na wananchi wenzao waliowafanyia wema kwa ajili ya Allah (s.w).
iv. Watoto wadogo watawashufaia wazazi wao waliokuwa wema kwao.