2 Kusimamisha Swala za Sunnah.
§
Umuhimu
wa Kusimamisha Swala za Sunnah.
a)
Kusimamisha swala za Sunnah ni kumtii na kumuiga Mtume
(s.a.w).
Rejea Qur’an (33:21) na (3:31).
b)
Hutupelekea kuwa Wacha-Mungu kwa njia nyepesi kupitia
utii na kujikurubisha zaidi kwa Allah (s.w).
c)
Hutupelekea kufikia lengo la swala kwa kujitakasa na
mambo machafu na mavu.
Rejea Qur’an (29:45).
d)
Swala za Sunnah pia hujaziliza mapungufu ya swala za
faradhi ambazo hazikuswaliwa kikamilifu kutokana na udhaifu wa kibinaadamu.
§
Aina za
Swala za Sunnah.
Rejea Kitabu cha 1, EDK, Shule za Sekondari ,
Uk . 150-165.
Swala za Sunnah ni nyingi, tutaangalia baadhi tu kama ifuatavyo:
i.
Swala ya Maamkizi ya Msikiti.
- Huswaliwa
rakaa mbili muda wowote mara tu muislamu aingiapo msikitini kabla ya kukaa.
ii.
Swala za Qabiliyyah na Ba’adiyyah.
- Hizi huswaliwa kabla
(Qabiliyyah) na Baada (Ba’adiyyah) ya swala za Faradh.
- Ziko aina mbili; ‘Mu’akkadah’
(zilizokokotezwa) na ‘Ghairu Mu’akkadah’ (Hazikukokotezwa).
Rejea
Kitabu cha 1, EDK, Shule za Sekondari ,
Uk . 152.
iii.
Swala ya Witiri.
- Huswaliwa
rakaa kwa idadi ya witiri; 1, 3, 5, 7, 9 na 11 katika theluthi ya mwisho wa
usiku au mara tu baada ya swala ya Ishaa.
- Witiri imekokotezwa mwisho wa
usiku zaidi na huambatanishwa kwa dua ya Qunuti katika rakaa ya mwisho.
iv.
Swala ya Tahajjud (Qiyaamul-layl).
- Huswaliwa
rakaa 8 usiku wa manane kwa rakaa mbili mbili na kumalia 3 za witiri na kutimia
rakaa 11.
- Huswaliwa
kwa kisimamo na kisomo kirefu cha Qur’an.
Rejea
Qur’an (17:79), (25:64), (39:9) na (73:1-4).
v.
Swala ya Tarawehe (Qiyaamu Ramadhan).
- Ni
swala ya kisimamo na Kisomo kirefu cha Qur’an, Juzuu 1 kila siku inayoswaliwa
mwezi wa Ramadhani tu baada ya Ishaa au kabla ya swala ya Alfajir.
- Kuna
hitilafu kwa idadi ya rakaa, kauli zinasema ni rakaa 8, 11, 20, 36, n.k.lakini
yenye nguvu ni rakaa 8 na 3 za witiri na kuwa jumla rakaa 11.
vi.
Swala ya Idil-Fitr na Al-Udhuhaa.
- Zote
huswaliwa rakaa mbili, Idil-Fitr huswaliwa mwezi 1 Shawwal baada ya kumalizika
funga ya mwezi wa Ramadhani.
- Idil-Al-Udhuhaa
huswaliwa mwezi 10 Dhul-Hija baada ya kukamilika ibada ya Hija kila mwaka.
vii.
Swalatudh-Dhuhaa.
- Huswaliwa
kila siku baada ya Jua kupanda kiasi cha mita tatu kutoka kuchomoza kwake.
- Huswaliwa
rakaa mbili mbili hadi kutimia nane, lakini kwa uchache huswaliwa rakaa mbili.
viii.
Swalatul-Istikharah.
- Ni
swala inayoswaliwa muda wowote kwa ajili ya kuomba msaada na mwongozo kwa Allah
juu ya uamuzi au utatuzi wa jambo lolote zuri.
ix.
Swala ya Kukidhi Haja.
- Ni
swala inayoswaliwa muda wowote kwa ajili ya kuomba msaada au utatuzi wa tatizo
lililotokea au unalohitajia.
x.
Swalatut – Tawbah.
- Huswaliwa
rakaa mbili muda wowote kwa ajili ya kutubia baada ya muislamu kufanya kosa.
Rejea
Qur’an (3:135-136).
xi.
Swala ya Kupatwa kwa Jua na Mwezi.
- Huswaliwa
kwa jamaa, rakaa mbili, rukuu mbili kwa kila rakaa moja. Huswaliwa kwa kisimamo
na kisomo kirefu mpaka Kupatwa kuondoke.
xii.
Swala ya Kuomba (Swalatul-Istisqaa).
- Ni
swala ya rakaa mbili kwa ajili ya kuomba mvua baada ya kuzidi dhiki na ukame,
kwa jamaa na uwanjani.
- Swala hii ina
khutuba mbili na takbira kama inavyoswaliwa
swala za Idi.