FAIDA NA MATUMIZI YA MISK:
Hali yake ina ujoto na uyabisi katika daraja la pili. Ina
ladha na harufu tofauti na mafuta mengine mazuri. Inatokana na mnyama anaeitwa
kwa kiarabu AL GHAZALI. Namna ya kutofautisha Misk halisi na feki ni kwa kuonja
ladha yake na kunusa harufu yake. Pia njia nyingine ni kwa kusomea aya za Ruqya
kwenye misk halisi halafu ajipake mwenye matatizo ya majini, italeta athari na
kama ni misk feki haiwezi kuleta athari. Vile vile misk feki haiwezi kutibu
maradhi ya kimwili kama vile maradhi ya ngozi.
MATUMIZI YA MISK KATIKA TIBA:
1) UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU: Kuna tiba iitwayo kitaalamu
Aromatherapy. Maana yake ni kupata dawa kwa njia ya kunusa au kupata harufu
yake kama vile kufukiza udi, misk huchangamsha ubongo na kuipa nguvu mishipa ya
fahamu. Utakuwa unanusa misk mara kwa mara au upate mvuke wake. Kwa kupata
mvuke wake chukua bakuli halafu uweke ndani yake maji ya moto yaliyochemka
halafu uweke ndani yake matone kadhaa ya misk. Sogeza bakuli karibu ya usoni
mwako ili upate kuvuta mvuke wake. Hali kama hii, mvuke wa misk utakuingia
kupitia puani au mdomoni. Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Ni nzuri kwa watu
wenye kifafa, dege dege, kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kutopata usingizi na
kuondosha kichefuchefu. Pia huongeza kumbu kumbu.
2) RHEUMATISM: Ni dawa ya kuondosha maumivu ya miguu, ganzi
na viungo. Ule ujoto wa misk huondosha maumivu ya mishipa, viungo, miguu,
mgongo na kiuno.
3) MZUNGUKO WA DAMU: Husaidia mzunguko wa damu na kuondosha
presha.
4)Kwa mwanamke inazidisha hisia na hamu ya tendo la ndoa.
5) HUONDOSHA HARUFU MBAYA: Kwa kuondosha harufu mbaya
makwapani au miguuni, jipake misk.
6) FANGASI SEHEMU ZA SIRI: Huondosha sehemu za siri
mwashowasho, mapele na harufu mbaya.
MATUMIZI YA MISK KWA KUMDHOOFISHA AU KUMFUKUZA JINI WA
MAHABA:
Kwanza kabisa misk isomewe aya za Ruqya, kisha mgonjwa
mwenyewe ajipake kila siku asubuhi na jioni viungo 32 vya mwili wake.
-Tundu mbili za pua.
-Tundu mbili za masikio.
-Kope mbili za macho.
-Mdomoni kama vile mfano wa lipstiki.
-Chuchu mbili (mwanamke anaenyonyesha asipake)
-Sehemu za siri mbele na nyuma.
-Kitovuni.
-Mbele mwa kucha zote za vidole 20 vya mikono na miguu.
TAHADHARI:
Ikiwa misk ni feki faida zote hapo juu za tiba haziwezi
kupatikana.
REFERENCE
1.http://mzizi-mkavu.blogspot.com/2014/06/faida-na-matumizi-ya-mafuta-ya-miski.html