Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo EDUCATION. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo EDUCATION. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 17 Aprili 2020

Maajabu ya Cheetah mnyama anayekwenda mbio zaidi kuliko wanyama wote nchi kavu.




Maajabu ya Cheetah mnyama anayekwenda mbio zaidi kuliko wanyama wote nchi kavu.
Huyu ni katika wanyama jamii ya paka, na anafanana zaidi na mnyama anayeitwa puma. Cheetah ni mnyama mwindaji kama walivyo chui, simba na mbwa mwitu. Ijapokuwa cheetah wanafanana kwa sura na maumbile lakini unaweza kutofautisha mmoja kwa mwingine kwa kutofautisha rangi za kwenye mikia yao.

Jumapili, 22 Machi 2020

KAZI ZA PROTINI MWILINI

PROTINI NI NINI?
Neno Protini asili yake ni kutoka katika lugha ya kigiriki  ”prōteios” na kwa kiingereza protein. Neno hili limeanza kutumika karne ya 19 mnamo miaka ya 1838 na Mkemia kutoka Swedish aliyetambulika kama Jöns Jacob Berzelius. Protini ni katika viinilishe muhimu sana ndani ya miili yetu. miili yetu haina uwezo wa kuhifadhi protini hivyo endapo itakuwa nyingi itabadilishwa kuwa fati na kupelekwa maene mengine ya mwili.

Jumanne, 17 Desemba 2019

FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA PILIPILI (kuzuia saratani, kisukari, maradhi ya moyo, kuimarisha ubongo)

14.Pilipili kali. Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi.

Jumanne, 1 Oktoba 2019

VIDONDA VYA TUMBO

 https://www.bongoclass.com

                      VIDONDA VYA TUMBO
Ni vidonda vinavyotokea katika ukuta wa tumbo. Vidonda hivi tumezoea kuviita vidonda vya tumbo ila hapa nitataja kitaalamu kuwa vidonda hivi hufahamika kama peptic ulcers. Vidonda hivi hutokea kutokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa H.pylori au kulika kwa ukuta wa tumbo kutokanana na athari za tindikali zilizopo tumboni (stomach acids) kama vile tindikali ya hydrocloric yaani hydrocloric acid. Kwa wakati tulio nao hili ni tatizo la kawaida maana limewapata watu wengi na halisabababishi vifo vya watu wengi kama maaradhi ya saratani na kisukari.

Vidonda hivi vimegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni:-
1.gastric ulcers hivi hutokea ndani ya tumbo la chakula
2.Esophageal ulcers hivi hutokea ndani ya esophagus. Hii ni sehemu inayounganisha kati ya koo la chakula na tumbo la chakula.
3.Duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum

Sababu za kutokea vidonda hivi
1.mashambulizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori (H.pylori). Hawa bakteria wanaweza kusabababisha mashambulizi na kuathiri sehemu tajwa hapo juuu na kusababisha vidonda hivi.
2.Matumizi ya baadhi ya aina za madawa mara kwa mara. Kuna aina za dawa ambazo kwa sasa zimepigiwa marufuku lakini hutumika kwa njia za panya. Madawa haya huweza kusababisha vidonda hivi kwa mfano aspirin, ibuprofen  na naproxene n.k
3.Uvutaji wa sigara
4.Kunywa pombe kupita kiasi
5.Athari ya miozi
6.Saratani ya tumbo
7.Misongo ya mawazo (stress)
8.Kukaa na njaa kwa muda mrefu.

DALILI ZA VIDONDA HIVI.
Dalili hizi hutofautiana kulingana na aina za vidonda. Ila hapa nitaorodhesha baadhi ambazo ni kawaida kwa vidonda hivi.
1.maumivu ya tumbo kutokea kitomvuni mpaka kifuani
2.Kukosa hamu ya kula
3.Kutoka na damu na kupata choo cheusi sana
4.Kupungua uzito bila sababu
5.Kutapika
6.Maumivu ya kifua
7.Tumbo kujaa.
8.Kuchoka ana

KUTHIBITI VIDONDA HIVI
1.wacha au punguza kunywa pombe
2.Usichanganye vilevi na madawa mengine
3.Punguza kutumia madawa aina ya aspirin n.k
4.Osha mikono yako mara kwa mara kuepuka maambukizi ya bakteria
5.Punguza misongo ya mawazo
6.Kula katika muda uleule.

Vidonda vya tumbo vinatibika bila ya shaka. Mgonjwa amuone mtaalamu wa afya na atimize masharti na ale dozi kulingana na kipimo husika. Pia kama sehemu imeharibika sana mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji. Kwa ambaye aansumbuliwa na vidonda hivi anashauriwa pia anywe maziwa.

Jumapili, 18 Agosti 2019

MAAJABU YA TEMBO

Mwandishi: Rajabu Athuman
Phone:     bofya hapa

5.SAFARI YA DAMU KWA KILA SIKU.
Damu ni tishu iliyopo katika hali ya kimiminika. Bila ya damu mwanadamu hawezi kuishi. Moyo ndio kiungo kikuu wenye mwili chenye kazi ya kuisambaza damu mwili mzima. Ukubwa wa kiungo hichi hufanana na ngumi. Moyo husafirisha damu kwenye mishipa inayokadiriwa kuwa na urefu wa kilomita elfu tisini na saba (97) na hii hufanyika ndani ya sekunde 20 tu.

Ijumaa, 26 Julai 2019

FAIDA ZA KARANGA

                        FAIDA ZA KARANGA


16. Karanga (ground nuts)
Karanga ni katika vyakula vya asili na ni kiungio cha mboga kwa jamii nyingi sana Tanzania na dunia kwa ujumla. Kama vilivyo vyakula vingine karanga ni katika vyakula vyenye virutubisho vingi. Ndani ya karanga kuna fotale, vitamin E, madini ya copper na arginine. Pia karanga ni chanzo kizuri cha omega-3 fatty acid, vitamin E na ijulikane kuwa fatty acid ni muhimu sana kwa afya ya moyo.