Jumapili, 2 Julai 2017

SWALA YA IJUMAA

Sala ya Ijumaa
Imeitwa Sala ya Ijumaa kwa vile inasaliwa siku ya Ijumaa, au kwa yale ya kheri yaliomo kwenye siku hii. Sala ya Ijumaa ni bora yao ya Sala na siku ya Ijumaa ni bora yao ya siku. Hivi ni kwa qauli ya Mtume  s.a.w.:

"Bora ya siku zilizochomoza jua juu yake ni siku ya Ijumaa, siku hio ameumbwa Adam a.s., na siku hio ametiwa Peponi, na siku hio ametoka Peponi, wala hakitasimama Qiyama isipokuwa siku ya Ijumaa". (Imehadithiwa na Muslim na Abu Daud na Al Nissaai na Al Tirmidhy).
Hukmu Yake
Sala ya Ijumaa ni waajibu kwa Qauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, qauli ya Mtume s.a.w. na itifaqi ya wanazuoni. Ametwambia Mwenyezi Mungu Mtukufu:
 "Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara ……". (Al Jumu'a : 9).
Na amesema Mtume s.a.w.:

HISTORIA FUPI YA PALESTIA

Muhammad Al-Ma’awy



Ulimwengu wetu wa sasa umekuwa ni wa utandawazi (ulimwengushi) kwa kiasi ambacho yaliyo ndiyo yamekuwa siyo na ya makosa yamechukuliwa kuwa ni ya makosa. Ulimwengu umekuwa ukipigwa makombora na vyombo vya habari kwa njia moja au nyingine.

Mwenye kumiliki chombo cha habari cha kilimwengu anaweza kupeperusha au kuandika ya kwake na yakaweza kuchukuliwa kama ukweli mtupu. Ulimwengu umekuwa ni wenye kuchukua yote na wenye sauti kubwa kwa kuwa na vyombo hivyo wameweza kusikika mbali  japokuwa hawana haki wa kupata wanayopata.

Kadhiya moja ambayo imeeleweka sivyo ni kadhiya ya historia ya Palestina. Waliojizatiti kuiweka katika hali hiyo iwe hivyo ni WAZEYUNI bila kuwa na pingamizi kwa kuwa na sauti kubwa. Juhudi dhidi yao zimekuwa zikifanywa bila ufanisi wowote kwa sababu ya sauti kubwa waliyonayo wao. Taasisi kubwa na maarufu za vyombo vya habari zinamilikiwa nao kwa namna moja au nyingine. Mbali na hiyo hatufai kufa moyo kuhusu juhudi hizo kwani nusura hutokea baada tawfiki ya Allaah Aliyetukuka, kisha juhudi zetu kwa kutumia njia tofauti.