Ijumaa, 12 Januari 2018

ADABU ZA DUA

 ADABU ZA DUA
Asalaamu alykum warahamatullah wabarakaatuh. Sifanjema sinamstahiki Allah Mola wa ulimwengu. Rehema na amani zimuendee kupenzi cha Allah mtume Muhammad (s.a.w).
Ama baada ya shukran hizi, katika darasa la leo tutaona baadhi ya adabu za kuomba dua. Itambulike kuwa dua ili ikubaliwe kwa urahisi ni lazima kumshawishi Allah akukubalie na hapa tunahitaji kutumia adbu za kuobea dua.  Kama ilivyo kawaida kun a utaratibu wa kila jambo. Hivyo jifunze leo adabu za kuoomba dua  kama ifuatavyo;-
1. Kuelekea kibla;
hivi ndivyo mtume alikuwa akiombaga duwa. Amepokea imamu bukhari hadithi kutoka kwa Abdallah Ibn Zaid kuwa mtume aliomba dua ya mvua akiwa ameelekea kibla. Kunyanyua mikono wakati wa kuomba dua.  Mapokezi ya imamu Bukhari kutoka kwa Abuu Musa; mtume alikuwa akiomba duwa hunyanyua mikono yake mpaka weupe wa kwapa huonekana.
2.Kuanza na kumhimidi Allah kisha na kumswalia mtume (s.a.w)
3.Kuwa na yakini na kujibiwa kwa duwa yako.
Hapa inahitajika kwa muombaji wa duwa awe na yakini kuwa du wa yake itajibiwa. Ni vizuri kuomba jambo ambalo moyo wako hautosita juu ya uwezekana wa kujibiwa. Katika mapokezi ya imam Tirmidhy na Alhaakim ni kuwa Mtume (s.a.w) amesema kuwa “muimbeni Mola wenu mlezi makiwa mnayakini ya kujibiwa…..” Usiharakishe malipo. Yaani usiharakishe kutaka kujibiwa mapema.
Ujuwe kuwa majibu yana jibiwa kwa njia nyingi pitia post zetu njia 3 ambazo dua hijibiwa. Pia hutokea majibu yakachelewa.
5.Kufanya yaliyo ya wajibu.
6.kujiepusha na mambo ya haramu
7.Kutaharisha tumbo yaani kula na kunywa vilivyo halali.
Kwa ufupi hizo ni baadhi tu ya adabu za dua. Pia itambulike kuwa  duwa pia zina nyakati na taratibu maalum ambazo zikifanywa hufanya duwa ijibiwe. Pia kuna duwa maalum ambazo ni zenye kujibiwa pasi na kizuizi. Katika post zijazi in shaa Allah tutazungumzia hili kwa undani.


>> fuata link zifuatazo ili uweze kupata update zetu.
>>> Bofya hapa kuungana nasi youtube ili upate video zetu nyingine

>>> Bofya hapa kupata masomo zaidi ya afya ukiwa na app yetu

>>> Ungana nami kwenye FACEBOOK

>>> Bofya hapa kupata yanayojiri katika blog hii