Jumatano, 17 Januari 2018

NYAKATI AMBAZO DUA HUJIBIWA KWA URAHISI.

Asalaamu alykum. Sifanjema zimuendee Allah. Sala na slamu zimfikie kipenzi cha Allah mtume muhammad (s.a.w). Ama baada ya maneno haya. Huu ni muendelezo katika darsa la dua. Kama tulivyoona darsa lililopita adabu za dua. Leo tutaona nyakati ambazo dua hujibiwa.
Hapa tutaangalia nyakati maalum ambazo kwa nyakati hizo mwenyekuomba dua haitarudi bure. Nyakati hizo ni;-
1.Theluthi ya mwisho ya usiku.
Katika mapokezi sahihi Allah hushuka mpaka mbingu ya dunia itakapofika thiluthi ya mwisho ya usiki. Kisha anasema " nani ataniomba nimpe(anavhotaka)....."
2.Dua baada y swala ya faradhi ni yenye kujjbiwa.

Baada ya kumaliza kuswali sio jambo la busara kuondoka bila ya kuomba dua. Kwani Mtume anatuambia kuwa dua inayoombwa baada ya swala ya faradhi ni yenye kunibiwa. ( amelokea tirmidhy kwa sanad hasan)
3. Dua kati ya adhana na iqama.
Kutokakwa anas mtume amesema "hairudishwi dua (inayoombwa) kati ya adhana na iqama. ( wamepokea hadith ashabu sunan kwa hasan).
4.Dua katika sijda.
Mtume amesema mtu anakuwa karibu zaidi na Allah anapokuwa amesujudi. Hivyo zidosheni dua mkiwa kwenye sijda.
5. Siku ya ijumaa kuna muda mchache ambao dua hairudi tupu.
Muda huu haujulikani na kuna kauli nyinhi sana. Wapo wanasema ni baada ya swala ya alasr mpaka magharib.
Jambo la msingi hapa soku nzima ya ijumaa tumuombe Allah huenda maombi yetu yakaagikiana na muda huo.
Huu ndio mwisho wa darsa la leo. Usikose darsa ijayo tutaangalia dua maalum ambazo huzijbiwa nola pazia.
Uanweza kupata habari zetu mpa moja kwa moja ukiwa na android app yetu. Ingia playstore kisha search MSAUD DUCE kisha instal
        <<<link muhimu>>>
>> fuata link zifuatazo ili uweze kupata update zetu.
>>> Bofya hapa kuungana nasi youtube ili upate video zetu nyingine

>>> Bofya hapa kupata masomo zaidi ya afya ukiwa na app yetu

>>> Ungana nami kwenye FACEBOOK

>>> Bofya hapa kupata yanayojiri katika blog hii