Jumamosi, 27 Januari 2018

DUAZA WATU HAWA NI ZENYE KUJIBIWA.

Asalaamu alykum warahmatu-Llah wabarakaatuh. Sifa njema zimuendee Allah mola wa ulimwengu. sala na salamu zimfikie kipenzi cha Allah mtume Muhammad(swala-Llahu alyh wasalam). ama baada ya utangulizi huu mfupi, tumeona katika darsa zilizopita kuhusu dua, adabu zake, mashart yake na nyakati ambazo dua hujibiwa.

Leo tutajifunza hali ambazo hupelekea dua kujibiwa. Na hapa hasa tutaangalia dua maalum ambazo hizo hujibiwa ima kwa kuambatana na hali flani au kutegemea na mazingira ya kuombaji au muombewaji dua.



1.Watu walio mbali wakiombeana dua hii itajibiwa.
Chukulia mfano watu wapo miji tofauti wakawa wanaombeana dua , dua hii ni yenye kujibiwa.
Imepokewa hadithi kuwa mtume amesema .." hakika dua iliyo rahisi kujibiwa ni dua (wanayoombeana) watu walio mbalimbali. ( ameipokea Tirmidh na Abuu Dawd kwa sanad sahih).

2.Dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa ni zenye kukubaliwa.
Watu watatu hawa Allah husikiliza dua zao naa huzijibu pasi na pazia. Yaani kwa namna yeyote ile dua hizi zitajibiwa tu. Amesimulia Abuuh-rairah kuwa Mtume amesema: "Dua za watu watatu ni zenye kujibiwa na hakuna shaka juu ya hili: dua ya mzazi, dua ya msafiri na dua ya mwenye kudhulumiwa. (ameipokea Abuu Dawd, Ahmad na Tirmidhy kwa sanad sahihi)

3.Dua ya mwenye funga (aliyefunga), imam muadilifu, na mwenye kudhulumiwa ni zenye kujibiwa.
Kiongozi muadilifu na mtu aliyefunga dua zao hazina pazia ni zenye kujibiwa. Na mwenye kudhulumiwa kama tulivyoona hapo juu.
Mtume Muhammad (swala-Llahu alyh wasalam) amesema: watu watatu hazirudishwi (bila ya kujibiwa) dua zao : mwenye funga mpaka afuturu, na imam muadilifu (kiongozi muadilifu) na dua ya mwenye kudhulumiwa...." ( ameipokea Tirhidhy kwa sanad sahih).

Kwa ufupi darsa letu litaishia hapa. Tumeona msafiri, mzazi, mwenye kudhulumiwa, kiongozi muadilifu, watu walio mbali wakiombeana dua na mwenye kufunga dua zao hazirudi. In shaa Allah darsa linalofata la dua tutaona matamshi maalum ambayo ukiyatumia kwenye dua yako dua hiyo itajibiwa bila ya shaka.
       WALLAHU A'ALAM

  Usiwache kuwa nasi katika post zetu nyingine 
>>> Kupata update zetu fuata link zifuatazo.<<<
>>> Bofya hapa kupata yanayojiri katika blog hii

>>> Bofya hapa kuungana nasi youtube ili upate video zetu nyingine

>>> Bofya hapa kupata masomo zaidi ya afya ukiwa na app yetu

>>> Ungana nami kwenye FACEBOOK