hapari ya saaizi ndugu msomaji. huu ni katika mwendelezo wa post zetu zinazolenga kuelimisha jamii kuhusu maswala ya kiafay. leo tutaangalia ugojwa hatari wa UTI na athari zake. ugonjwa huu umejichukulia umaarufu kwa kifingi cha miaka michache ya hivi karibuni. unaweza kusoma posti zetu zote zinazohusu afya ukiwa na program zetu za simu. bofya hapa kudownload program zetu. pia unaweza kutupata kwenye youtube bofya hapa.
UTI ni kifupisho cha Urinary Transmission Infection. Ni ugonjwa unaoshambulia katika mfumo wa mkojo, hususan kibofu, figo na mirija ya urethra. Ugonjwa huu umekiwa ukiwapata sana wanawake kwa kiasi kikubwa kuliko wanaume. Baadhi ya takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu 5 mmoja ana UTI.
UTI ni kifupisho cha Urinary Transmission Infection. Ni ugonjwa unaoshambulia katika mfumo wa mkojo, hususan kibofu, figo na mirija ya urethra. Ugonjwa huu umekiwa ukiwapata sana wanawake kwa kiasi kikubwa kuliko wanaume. Baadhi ya takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu 5 mmoja ana UTI.
Maambukizi ya ugonjwa huu yanapatikana hasa chooni. Pia huenda ugonjwa huu ukaenezwa kupitia kuingiliana kimwili na utaratibu mbovu wa kujisafisha baada ya kukidhi haya. Ugonjwa huu umekuwa ukiwapata zaidi watu ambao wanatumia vyoo vya shirika yaani vyoo vinavyotumiwa na watu wengi.
Ugonjwa wa UTI umekuwa ukisababishwa na bakteria kwa kiasi kikubwa. Bakteria aina ya E.coil ambao wanapatikana kwenye utumbo mkubwa wamekuwa wakisababisha UTI kwa kiasi kikubwa kuliko bakteria wengine. Pia fangasi (fungi) na virusi huweza kusababisha UTI japo kwa kiwango kidogo.
Mtu anaweza kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa huu kwa,;-
1. Jisafishe kutokea mbele kuelekea nyuma baada ya kukidhi haja kubwa (kwa wanawake). Hii husaidia kuzuia bakteria wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wasipate nafasi ya kuingia kwenye njia ya haja ndogo.
2. mwaga maji kila uingiapo chooni kwaajili ya nkujisaidia. Kitendo hiki kitaondosha vijidudu vilivyopo pale chini.
3. Jisafishe sehemu za siri kabla ya kuingiliana na baada.
4. Hakikisha unakwenda kutoa haja ndogo (kukojoa) baada ya tendo la ndoa. Kitendo hiki kitasaidia kuondosha vijidudu vilivyoingia wakati wa tendo.
5. Nenda katoe haja ndogo haraka sana baada ya kuhisi.
6. Kunywa maji mengi zaidi. Husaidia kuondowa vijidudu kwa njia ya mkojo.
7. Vaa nguo za ndani za pamba, kavu na zisizobana.nguo za mpira na zinazobana husababisha jasho (majimaji) sehemu za siri. Majimaji haya husaidia bakteria kukuwa na kuishi hivyo wanaweza kuathiri njia ya mkojo.
Ugonjwa wa UTI una dalili nyingi na huenda nyingine zikafanana na dalili za malaria. Miongoni mwa dalili hizi ni;-
1. Maumivu wakati wa haja ndogo
2. Kutowa mkojo mchafu. Mkojo unawea kuwa na rangi sana, ua kama wa mawingu na kadhalika.
3. Harufu kali sana ya mkojo.
4. Mkojo kuwa na damu
5. Kukojoa marakwa mara hata kama mkojo utakuwa ni mchache sana.
6. Maumivu ya mgongo na tumbo kwa chini.(lower abdomen)
7. Maumivu ya kichwa.
8. Kuhisi uchovu sana
9. Miwasho sehemu za siri.
Itambulike kuwa ugonjwa wa UTI unatibika bila ya matatizo. Jambo la msingi ni kuwa wagonjwa wengi wamekuwa hawamalizi dozi. Kwakuwa ugonjwa huu umeenea sana na ni rahisi kuupata imetokea hali za kujirudia rudia. Hivyo mgonjwa ni muhimu kuchukuwa tahadhari tulizotzja hapo juu wakati akiwa anatumia dozi. Pia watu wawe makini na tiba za kiasili ambazo husemekana zinatibu UTI.
>>> HAYA NA MENGINEYO UTAYAPATA UKIWA NA APP YETU<<<>>> Bofya hapa kupata APP yetu
>>> Bofya hapa kuungana nasi youtube ili upate video zetu nyingine
>>> Bofya hapa kupata masomo zaidi ya afya ukiwa na app yetu
>>> Ungana nami kwenye FACEBOOK