Kupanga Uzazi katika Uislamu
Kama ilivyo haramishwa kwa jamii, Uislamu umeharamisha pia
kudhibiti uzazi kwa mtu binafsi kwa khofu ya kushindwa kuwalisha au
visingizio vingine. Hata hivyo Uislamu haujawataka watu wazae kiholela.
Kwanza umekataza watu kuzaana nje ya ndoa. Pili, walioona
wanatakiwa wazingatie umri baina ya mtoto na mtoto mwingine. Kwa
anayetaka kukamilisha muda wa kunyonyesha, basi amnyonyeshe mtoto
wake kwa miaka mwili kama Allah anavyotuambia
Na wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili
kamili, kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha…” (2:233)
Kunyonyesha humsababisha mama mzazi kuchukua muda mkubwa
kabla ya kuingia tena katika siku zake. Iwapo mwanamke atapata siku
zake wakati mtoto yungali mchanga (hajafikia umri wa miaka miwili),
anatakiwa ajizuie asipate mimba; kwani katika Hadith iliyosimuliwa na
Imamu Muslim, Mtume (s.a.w) amesema kuwa mwanamke akipata
mimba wakati yungali na mtoto mchanga, afya ya mtoto hudhurika.
Njia za kuzuia mimba katika kipindi hiki cha kunyonyesha ni zile ambazo
hazina madhara ya kiafya kwa baba wala mama. Katika Hadith
iliyopokelewa na Bukhari na Muslim, Jabir (r.a) amesema kuwa wakati wa
Mtume (s.a.w) wao walikuwa wanatumia njia ya kuzuia mimba inayoitwa
‘azal” (with drawal au coitus interuptus), yaani njia ya kumwaga mbegu za
uzazi nje lakini Mtume (s.a.w) hakuikataza.
Hapa ifahamike kwamba suala la kupanga juu ya muda wa
kunyonya mtoto linamhusu baba na mama na si suala la kuwekewa sera
na taifa; kwani hali za watu zinatafautiana.
Ama kwa mama atakayekuwa na matatizo ya kiafya, ikathibiti kuwa
akibeba mimba atadhurika au kuhatarisha maisha yake, anaruhusiwa
kufunga kizazi hata kutoa mimba ambayo imeshatunga
>>> Kupata update zetu fuata link zifuatazo.<<<>>> Bofya hapa kupata yanayojiri katika blog hii UKIWA NA APP YETU
>>> Bofya hapa kuungana nasi youtube ili upate video zetu nyingine
>>> Bofya hapa kupata masomo zaidi ya afya ukiwa na app yetu
>>> Ungana nami kwenye FACEBOOK