Alhamisi, 22 Machi 2018

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA sehemu ya kwanza

       
 
 KIAPO CHA SULTANI
Hapo zamani sana katika nchi za Uajemi , china na hindi kulitokea sultani aliyefahamika kwa kuwa na upendo kwa watu wake na nguvu pia ya kijeshi na kuitawala. Watu wake walimpenda sana na yeye aliwapenda. Sultani huyu alikuwa na watoto wawili ambao ni Shahriyar ambaye ndiye mkubwa na mwingine ni Shahzanam ambaye ndiye mdogo.

Watoto hawa pia walitambulika kwa ushujaa walio nao na uhodari katika mambo mbalimbali, hususan katika fani ya kupanda farasi. Sultani huyu alipofariki utawala wake akamwachia mwanaye mkubwa ashike madaraka yake. Na mwanae mdogo akabakia anatawala maeneo mengine katika utawala wa baba yake. Huyu mdogo akaelekea maeneo ya Samarkand na huyu mkubwa akabaki palepale.   bofya hapa


Sultan Shahriyar alikuwa na mke wake aliyempenda sana kwa muda mrefu. Hakuwahi kuamini kama itaweza kutokea sikumoja akamsaliti. Ilitokea sikumoja akamkuta mkewake anazini na mtumwa wake. Kitendo hiki kilimuuma sana na akamuuwa mkewe na yule mtumwa. Kutokea hapo akaapa kutokumwamini mwanamke yeyote duniani. Na kitendo hiki kilimfanya ajiwekee utataratibu mpya wa maisha nao ni kuoa kila siku mke mpya na kisha humuuwa ifikapo asubuhi.

Hivyo mambo yakawa kama hivi kila siku jioni bibi harusi mpya mwanamwari huolewa na na ikifika asubuhi huuliwa. Kitendo hiki kiliendelea kwa muda mpaka watu wakawa wanaogopa. Ikiwa nyumba moja watu wanalia kwa kufiwa na bint yoa nyumba nyingine hufanyika harusi. Sultani alikuwa na waziri wake maalum ambaye alikuwa amepewa kazi hii ya kumletea mfalme wanawari na kutekeleza amri ya kuwauwa kila ifikapo asubuhi.

Waziri huyu aliyepewa kazi hii alikuwa na watoto wawili aliyewapenda sana, mmoja aliitwa Schehra-zade ambaye ndiye mkubwa na Dinar-zade ambaye ndiye mdogo. Schehra-zade alipata upendo mkubwa kutoka kwa baba yake. Alipewa taaluma mbalimbali za matibabu, sanaa, kuandika, masimulizi , kazi za mikono na nyingine nyingi. Ukiacha mbali na taaluma hizi pia alijulikana kwa uzuri wake ulioaminika kuwashinda wanawake wote katika nchi hiyo. Mabinti wawili hawa walipendana zaidi kila mmoja.

Ilitokea siku moja katika mazungunzo waziri mkuu akiwa na mabinti zake wanaongea  Schehra-zade alitowa ombi kutoka kwa baba yake ambalo lilionekana kumshangaza sana.
“baba ninaombi ila niahudi kwanza kuwa utanitekelezea” alizungumza  Schehra-zade kumwambia baba yake. “naahidi nitalitekeleza kama lipochini ya uwezo wangu” alisikika waziri mkuu akimjibu binti yake.
“ninataka kukomesha tabia ya kikatili ya sultani kuuwa mabint” mmmmhhh mwanangu kipenzi, vip utaweza kumaliza tabia hii ya sultani wetu? Ni maneno yaliyokuwa yakizungumzwa kati ya waziri na mwanae. “baba ninataka unipeleke mimi kwa sultani niwe mkewe” alizungumza  Schehra-zade. Mwanangu unafahamu fika kuwa ukuolewa punde tu ifikapo asubuhi nitaamriwa nikuuwe” alizungunza waziri kwa masikitiko makubwa.

 Schehra-zade aliendelea kusisitiza ombi lake la kutaka kuolewa na sultani ili akamalize tabia yake ya kuuwa mabinti. Waziri nae hauacha kumsihi mwanae asithubutu kijiingiza kwenye matatizo haya makubwa. Wazii akawa anamwambia mwanae “ hivi mwanangu unataka nikufanye kitugani mpaka uachane na msimamo wako huo? Au unataka yakupate yalompata mke wa mfugaji?” kwa shauku  Schehra-zade akauliza “kwani baba ni kitu gani kilimpata mke wa mfugaji” mmmmhh.. Ni habari kubwa lakini nitatakusimulia hadithi yake” alizingumza waziri na kuanza kusimulia hadithi hii
kusoma hadithi hii yote bofya hapa
          KISA CHA MFUGAJI NA MKEWE.
Hapo zamani kulikuwa na mfugaji maarufu sana na alikuwa ni tajiri na mfanyabiashara aliyekuwa na mafanikio makubwa. Alikuwa anaelewa lugha za wanyama. Alipata tunu hii kwa sharti kuwa asisimulie kwa yeyote mazungumzo ya wanyama na pindi tu akisimulia alichokisikia atakufa hapohapo. Alikuwa akifurahia sana kuwaona wanyama wake na kujuwa nini wanazungumza. Alikuwa na banda lake la wanyama ambapo ndani kulikuwa na ng’ombe na punda, ambapo kazi ya kuwasimamia wanyama hawa alimpa mtumwa wake.

Sikumoja alipkuwa amekaa pembeni mwa banda hilo akasikia mazungumzo ya kustaajabisha kati ya punga na ngo’mbe. Ngombe akamwambia punda “ nakuonea wifu kwa raha unayoipata. Wakati mimi ninashinda juani kulima shamba la bwana wetu wewe mwenzangu unaogeshwa na kupambwa na kazi yako ni kummeba bwana wetu, wananipiga, wananifunga majembe yao shingoni. Nakuonea wivu natakani ningekuwa wewe” punda akamwambia ng’ombe “usijali nitakueleza jambo ukilifanya katu hautalimishwa tena.. Kesho akija mfanyakazi mpige mateke na mtishe kwa pembe zako na umfukuze. Kataa kula chakula chao. Ukifnya hivi katu hawata kulimishwa tena”

Siku iliyofuata ng’ombe akafanya kama alivyoshauriwa na punda, akamtisha mfanyakazi na akamkimbiza akataka kumchoma kwa pembe zake. Alikataa kula chakula. Siku iliyofuata mfanyakazi akakuta kile chakula alichokilet jana kipo vilevile hivyo akatoa taarifa kwa bwana wake. Mfugaji akamuamuru mfanyakazi wake amchukuwe punda kwenda kulima amfanyie mazoezi. Hivyo siku ile punda akapew mazoezi ya kulima na akalima pia kwa jembe la kubuluza (plau). Jioni akarudi akiwa amechoka sana.
kusoma hadithi hii hapa

Kufika hapa waziri akamwambia mtoto wake  Schehra-zade “binti yangu hivi unataka kuangamia kama punda alivyomshauri mwenzie vibaya na akaumia mwenyewe?”  Schehra-zade akamwambia baba yake “baba bado msimamo wangu upo pale pale nipeleke kwa sultani nikakomeshe tabia yake. Lakini baba bado sijajuwa mke wa mfugaji kilichompata?” alizungumza  Schehra-zade kutaka hadithi iendelee. Waziri akaendelea kumsimulia  Schehra-zade hadithi hii

Siki moja mfugaji akiwa na mkewe wameketi karibu na banda la wanyama hawa ili kujuwa nini punda atamshauri mwenzie. Akamsikia punda akimwambia ng’ombe “rafiki yangu nakupa ushauri unisikilize vizuri. Nimemsikia bwana wetu akimwambia mfanya kazi kuwa kama hali yako utaendelea nayo basi uchinjwe na upelekwe buxher ukauzwe nyama. Hivyo nakushauri kesho utii amri ya mfanya kazi hivyo atadhani kuwa ulukuwa umeumwa na sasa umepona” ngo’ombe alionekana kutii ushauri huu. Hapo mfugaji akacheka sanaa. Kicheko hiki kilistaajabisha hata mkewe. Mkewe akataka kujua kinachomchekesha akamjibu ni siri na nikikwambia nitakufa ila naweza kusema kuwa ninacheka kwa sababu ya mazungumzo kati ya punda na ng’ombe.

Mke huyu alionekana kuwa na msimamo wa kutaka kujuwa hasa nini mazungumzo hayo nini kilisemwa mpaka akacheka. Akaahidi kama asipomwambia atarudi kwao. Ugomvi ukawa mkubwa ikafikia hatuwa ya kuita ndugu waje kusuluhisha. Mfugaji akabaki na msimamo wake kuwa kama atasema atakufa paohapo na mke akafikia kusema kama asipi niambaia na mimi nitajiuwa. Hali hii iliendelea kwa muda mpaka kufikia hali mbaya zaidi. Mfugaji akiwaza nimwambie ili nife kwa kumridhisha mke wangu au nisimwambie. Na nisipo mwambia atajiuwa. Ni mawazo ya mfugaji. Ugomvi uliendelea kwa siku kadhaa bila ya maelewano pale ndani.

Siku moja alikaa nyumbani kwake ghafla akamuona mbwa wake aliyempenda sana anamkimbilia jogoo la kuku. Kisha akamuelezea mambo yote yaliyompata bwana wake yaani mfugaji na mkewe. Hapo jogoo akacheka sana kisha akamwambia “bwana wako ni mpumbavu kweli, hivi hauniono mimi nina wake zaidi ya hamsini hapa na ninafanya ninalo taka, lakini yeye ana mke mmoja tuu pia anampa wakatimgumu hivi. Akieleza siri atakufa hapa dawa ni ndogo tu. Achukuwe fimbo mzuuri kisha amtandike kisawasawa, bila shaka atarudisha akili yake.” Baada ya maneno haya jogoo likawika na kuondoka zake kwa mwendo wa madaha.

Mfugaji alifikiri atumie ule ushauri wa jogoo, asubuhi ya siku ilofata mke wa mfugaji aliendelea na vurumai lake. Mfugaji akaagiza aletewe bakora nzuri na kutekeleza ushauri wa jogoo. Mambo yakatulia nyumbani na hakuleta vurumai liole tena. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii waziri akamwambia Schehra-zade “binti yangu, je unataka na mimi nitumie uamuzi wa jogoo?” Schehra-zade akamwambia baba yake “hapana baba ila mi nadhani hadithi hii hainitoshelezi kubadili uamuzi wangu”. Basi waziri baada ya mazungumzo marefu akakubaliana na maamuzi ya mwanae na kukubali kumpeleka kuwa bibi harusi kwa sultan kwa usiku uliofuata. itaendelea aubofya hapa

kusoma hadithi hii yote bofya hapa