Jumatatu, 28 Mei 2018

SUNNAH ZA FUNGA (SWAUM)

           

 Sunnah za funga

1.kula daku.

Amesema Mtume: kuleni daku kwa hakika mna baraka katika kula daku (Bukhari na Muslim). Na kula daku sio lazima kukusanya mavyakula mengi na mazuri hapana,  Mtume (s.a.w) amesema: fanyeni daku japo kwa maji (Ibn Majah). Na bora ya daku ni kula tende kama alivyosema mtume katika hadithi aliyoipokea Abuu Daud nayo ni hadithi sahihi.





2.kuchelewa katika kula daku. Ni sunnah kuchelewa kula daku mpaka karibia na adhana ya alfajiri. Amesimulia Zaid Ibn Thabit kuwa tulikuwa tukila daku pamoja na mtume kisha kasimama kuiendea swala, akauliza Anas Ibn Malik kumuuliza Zaid: kulikuwa na urefu wa muda gani kati ya muda wa daku na adhana ya swala akasema Zaid: ni kiasi cha kumaliza kusoma aya 50 (za quran) (Bukhari na Muslim). Wakati huu kulikuwa na Adhana mbili katika swala ya lfajiri hivyo Mtume akawaambia Masahaba: atakapoadhini Ummul-maktum kuleni na kunyweni na atakapoadhini bilali msile wala msinywe.(Nisai).



3.Kuwahi kufuturu. Amesema Mtume: watu hawaachi kuwa wapo kwenye here maadamu wanawahi kufuturu. (Bukhari na Muslim). Yaani ni heri tupu inapatikana kwa kuwahi kuftari.

4.Kufuturu kwa kitu cha majimaji au kwa tende.amesimulia Anas kuwa alikuwa mtume anafuturu kwa kitu cha majimaji kabla ya kuswali na akikosa chenye majimaji basi hufuturu kwa tende na akikosa hufuturu kwa maji. (Abu Daud na tirmidh)

5.Kuomba dua wakati wa kuftari. Alikuwa Mtume akiomba dua hii “dhahaba dhw-dhwamau, wab-taliyatl-’uruuq wathabatil-ajru in shaa Allahu (Nisai)

6.Kujipinda katika kheri mbalimbali pamoja na kusoma qurani kwa wingi. Alikuwa Mtume anakundishwa qurani katika mwezi wa ramadhani

7.Kuacha maneno ya upuuzi,uongo na matendo machafu. Amesema Mtume mtu ambaye hawezi kuacha kuzungumza uongo na kufanyia kazi matendo ya uongo Allah hana haja na (funga yake mtu huyu.) kuacha chakula chake na kinywaji chake.(Bukhari)  Na katika maneno mengine mtume anakataza kwa mwenye kufunga kufanya uovu na uchafu mwingine.

Kuendelea na darsa bofya hapa