Alhamisi, 27 Septemba 2018

Sharti na Nguzo za swala



Sharti za Swala
Sharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali. Mambo haya ni:
 1. Twahara.
 2. Sitara.
3. Kuchunga wakati.
4. Kuelekea Qibla.



Zifuatazo ni nguzo za Swala:
 1. Nia - dhamira moyoni.
 2. Takbira ya kuhirimia (au Takbira ya kufungulia Swala).
3. Kusoma suratul-Fatiha.
 4. Kurukuu.
5. Kujituliza katika rukuu.
6. Kuitidali (kusimama kutoka katika rukuu).
7. Kujituliza katika itidali.
8. Kusujudu.
9. Kujituliza katika sijda.
10. Kukaa kati ya sijda mbili.
11. Kujituliza katika kikao cha kati ya sijda mbili.
 12. Kusujudu mara ya pili.
 13. Kujituliza katika sijda ya pili.
 14. Kukaa Tahiyyatu.
15. Kusoma Tahiyyatu.
16. Kumswalia na kumtakia rehema Mtume (s.a.w) na Waislamu.
 17. Kutoa Salaam.
 18. Kuswali kwa kufuata utaratibu huu (1 - 17).

 Nguzo hizi za swala tunaweza kuzigawanya kwenye makundi manne:
(a) Nia.
(b) Nguzo za matamshi (visomo)
(c) Nguzo za vitendo.
(d) Kufuata utaratibu. Katika nguzo 18,

nguzo za matamshi ni hizi tano zifuatazo:
(i) Takbira ya kuhirimia swala.
(ii) Kusoma suratul-Fatiha (Al-hamdu).
(iii) Kusoma Tahiyyatu.
(iv) Kumswalia Mtume.
(v) Kutoa Salaam.
Nguzo zote zilizobakia, ukiacha nia na kufuata utaratibu ni nguzo za vitendo.