Jumanne, 2 Oktoba 2018

USIVYO NA FADHILA

FACEBOOKUSIVYO NA FADHILA

Akusomeshe kwatabu, mateso yakukulea,
Mwana usivyo aibu, machafu wamtolea,
Kisha waona ajabu, maafa kukulemea,
Usivyo na fadhila

Wamuacha kijijini, bila yakumtazama,
Yakunoga yamjini, yakuondoka huruma,
Rafiki wawathamini, yeye wamuweka nyuma,
Usivyo nafadhila



Unajiona mwenyeji, mambo umejiwahia,
Una yavaa ya mji, nawatu wakusifia,
Hukumbuki mahitaji, yake kumtimizia,
Usivyo nafadhila

Anasa kwako fasheni, dharu ndo cheo chako,
Umesahau hisani, alizo zitenda kwako,
Bila yeye duniani, ivi ungelikuweko?
Usivyo nafadhila

Anaminyika najembe, masika vuli najoto,
Alima ili siombe, tadhani hana mtoto,
Wewe na wako wapanbe, mwajita watu wazito,
Usivyo nafadhila

Sauti yake nun'guno, anun'gunika kwa mengi,
Kwanza kile kiminyano, ukiwa shule msingi,
Akijinyima vinono, kukulipia shilingi,
Usivyo nafadhila,

Tabu zako utotoni, alivyo zivumilia,
Lake kubwa tumaini, kesho tamsaidia,
Ona sasa masikini, aambulia kulia,
Usivyo nafadhila

Usimtupe mzazi, vyovyote vile awavyo,
Yeye ndie yako ngazi, umtunze ipasavyo,
Na yeye ndio mzizi, wawewe leo ulivyo,
Zikumbuke fadhila

Mtunzi:HD.Hassan
@SUKARI YA MASHAIRI@
Pangani Tanaga
8/8/2018
02:12 asubuhi