Jumanne, 4 Februari 2020

VIJUE VIRUSI VYA KORONA AMA CORONA (CORONA VIRUS)

VIRUSI VYA KORONA (CORONA)
Corona ni virusi vinavyotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Virusi hivi vimeitwa corona kwa kwa kuwa vinafanana na taji (crown). Corona ni neno la kilatini lenye maana ya crown. Virusi hivi vimegunduliwa toka mwaka 2003 China na karibia watu 800 walifariki. Na mwaka 2012 nchini Saud Arabia virusi vya corona viligundulika tena na kusababisha vifo takriban watu 850. na sasa mwaka 2020 kwa mara nyingine nchini China virusi vya corona vimeibuka tena.



Virusi vya corona ni virusi ambavyo vinaathiri mfumo wa upumuaji. Virusi hivi huleta homa, kukohoa pamoja na kushindwa kupumua vizuri. Mpaka sasa kuna maradhi aina tatu ambayo hufahamika kuwa hiletwa na virusi vya corona. Magonjwa hayo ni kama:-
SARS yaani Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS-CoV) uligundulika China mwaka 2003 na kuuwa watu 800
MERS yaani Middle East Respiratory Syndrome (MERS-CoV) uligundukika Saud Arabia na kuuwa watu 850
2019-nCoV yaani 2019 Novel Coronary Virus (2019-nCoV) mpaka kufikia 3/2/2020 umeua watu 361

Virusi vya corona huenezwa kwa njia ya hewa na kugusana. Pindi mgonjwa anapokohoa ama kupiga chafya, anaweza kumuambukiza mtu mwingine kwa umbali wa futi 6. pia kwa njia ya kugusana kunaweza kueneza virusi hivi. Bado wanasayansi wanatafiti zaidi juu ya virusi hivi na njia hizi zinazosambaza virusi hawa.


Tafiti zinaonyesha kuwa virusi hivi china vilianzia kwenye vyakula vya baharini yaani samaki, na baada ya hapo ikaenea kwa watu kwa kupitia hewa na kugusana. Mpaka sasa hakuna chanjo ya virusi hivi na pia hakuna dawa maalumu kwa virusi hawa. Miongoni mwa njia za kujiepusha na virusi hivi ni kujiepusha kugusana na mgonjwa, kuosha mikono na sabuni kabla ya kula, baada ya kutoka chooni, baada ya kukohoa ama kupiga chafya.

 Soma zaidi makala za afya hapa