Jumanne, 3 Machi 2020

Makatazo juu ya kuisahau Quran baada ya kuihifadhi


Kama ilivyokuwa mahimizo juu ya kuisoma qurana mara kwa mara na kuihifadhi, hivyo hivyo imakatazwa kuiwacha quran na kuisahau baada ya kuihifadhi. Kuna nukuu mbalimbali zinazotutaka kuishika vizuri quran, na kutokuisahau baada ya kuhifahi hata iwe aya moja. Katika makala hii fupi tutakwenda kuona mahimizo hayo na kuangalia ni hukumu gani kwa atakayesahau quran.


Ndugu yangu muislamu, makala hii ni mwendelezo wa makala zetu za dini. Unaweza kupata makala nyingine za dini kwenye tovuti yetu www.bongoclass.com. unawza kutuunga mkono kwa kushea makala hizi ama kutusaidia kuedit makala hizi. Tunafanya kazi hii kwa ajili ya Allah na si vinginevyo.

Kama nilivyotangulia kusema kuwaMtume (s.a.w) amehimiza sana kuisoma qura mara kwa mara. Hii ameisema ili tukifanya hivi katu hatutaweza kuisahau quran baada ya kuihifadhi.

عَنْ أَبي مُوسَى رضِيَ اللَّه عنهُ عن النَّبِيِّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » تَعاهَدُوا هذا الْقُرآنَ فَوَالَّذي نَفْسُ مُحمَّدٍ بِيدِهِ لَهُو أَشَدُّ تَفَلُّتاً مِنَ الإِبِلِ في عُقُلِها « متفق عليه
Imepokewa Hadith kutoka kwa Abuu Musa kuwa Mtyme (s.a.w) amesema: “isomeni quran mara kwa mara kwani kwa hakika naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo Mikononi mwake, (hiyo quran) inakimbia haraka (kutoka kwenye moyo bada ya kuhifadhiwa) kuliko ngamia (anavyokimbia) kwenye kamba aliyofungiwa” (Bukhari na Muslim)

Katika hadithi hii tunajifunza mambo kadhaa:
1. Tunatakiwa kuisoma quran mara kwa mara
2. Quran tutaweza kuisahau kwa haraka sana kama hatujaisoma mara kwa mara.

Katika mapokezi mengine Mtume (s.a.w) anatueleza:
عنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِي اللَّه عنهما أَنَّ رسولَ اللَّه صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » إِنَّمَا مَثَلُ صاحِبِ الْقُرْآنِ آَمَثَلِ الإِبِلِ المُعقَّلَةِ ، إِنْ عَاهَد عَليْها أَمْسَكَهَا ، وإِنْ أَطْلَقَهَا ، ذَهَبَتْ « متفقٌ عليه
Imepokewa Hadith kutoka kwa Ibn ‘Umar kuwa Mtume (s.a.w) amesema “Mfano wa mtu aliyehifadhi quran ni sawa na mfano wa mtu mwenye ngamia, akimfunga vyema ataweza kuwa naye lakini akimuachia atakwenda (mbali).

Maana ya Hadithi hii na iliyotangulia zinafanana, zote zinatutaka kuisoma quran mara kwa mara ili kutokuisahau. Miongoni mwa njia za kutufanya kuisoma quran mara kwa mara ni kuisoma kwenye visimamo vya usiku. Mtume (s.a.w) alikuwa akisoma surat albaqara nzima na zaidi katika swala za usiku.

JE KUNA MADHAMBI KWA KUISAHAU QURAN?
Kusahau ni jambo la kawaida kwa Mtu yeyote. Mtume (s.a.w) ameeleza kuwa mwanadamu ameitwa “insan” kutokana na sifa yake ya kusahau. Hivyo kusahau ni sifa za binadamu. Unaweza kusahau hata muda wa swala na ukaruhusiwa kuiswali pindi utakapokumbuka. Hivyo Allah katu hataweza kutuadhibu kwa kusahau huku.

Maulamaa kama Imam Suyut na Imam Nawaw wanamsimamo kuwa ni katika madhambi kuisahau quran. Mtazamo huu wanaupata kutokana mapokezi ya baadhi ya hadithi.

Imepokewa hadithi kutoka kwa Anas Ibn Maalik (r.a) ambaye amesema: ‘nilionyeshwa madhambi ya ummati wangu, na sikuona dhambi kubwa zaidi ya dhambi la mtu ambaye mepewa (amesaidiwa kuhifadhi) sura ama aya katika quran kisha akaisahau” uchambuzi wa hadithi hii unaonyesha kuwa hadithi hii ni dhaifu. Ameitaja imam Tirmith na imam Bukhari kuwa hii hadithi ni dhaifu, na pia Imam Al-Alban ameitaja kuwa ni dhaifu. Na itambulike kuwa hadithi dhaifu hazitumiki katika kutoa hukumu za kisheria.

MWISHO:
Ijapokuwa hadithi iliyotajwa ni dhaifu lakini ni vizuri tukajitahidi kuisoma quran mara kwa mara na tujitahidi tusiisahau. Kwani kuna fadhila nyingi sana za quran hasa kwa wale ambao wameihifadhi katika vifua vyao. Unaweza pia kupata makala zetu nyingine kwenye tovuti yetu. Makala nyingine unazoweza kupata ni kama:

2. Darsa za swala
3. Darsa za quran
4. Darsa za afya ya uzazi
5. Darsa za tajwid.