Jumanne, 3 Machi 2020

Ni zipi Fadhila za kusoma na kusikiliza Quran


Ni zipi Fadhila za kusoma na kusikiliza Quran

Quran ni kitabu cha Allah kinachotoa mafunzo katika sheria, makatazo na maamrisho na mengineyo mengi. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya kiarabu, hivyo huwafanya watu wajifunze kusoma kiarabu ndipo waweze kusoma quran kiusahihi zaidi. Kitabu hiki pia kinaweza kuhifadhiwa hata kabla ya mtu kuweza kujua kusoma maandishi ya kiarabu.


Changamoto ya wasomaji wengi leo hawajui faida za kusoma quran. Tutakwenda kuona fadhila kuu 9 zinzopatikana katika kusoma quran. Chini hapo nitataja baadh tu ya faida za usomaji wa quran, katika makala hii nitakwenda kukueleza miongoni mwa faida hizo:-

1. Quran ni kiombezi siku ya kiyama kuja kumuombea mtu wake aliyeisoma quran duniani;
Mtume Muhammad (s.a.w) amesema kuwa “somenu quran kwani hakika ya hiyo quran italetwa siku ya qiyama kuja kumuombea mtu aliyekuwa akiisoma” (Muslim)
عن أَبي أُمامَةَ رضي اللَّه عنهُ قال : سمِعتُ رسولَ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : » اقْرَؤُا القُرْآنَ فإِنَّهُ يَأْتي يَوْم القيامةِ شَفِيعاً لأصْحابِهِ « رواه مسلم

2. Mtu mwenye kusoma quran na kuifanyia kazi ndiye mtu bora

عن عثمانَ بن عفانَ رضيَ اللَّه عنهُ قال : قالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : » خَيرآُم مَنْ تَعَلَّمَ القُرْآنَ وَعلَّمهُ رواه البخاري

Imepokewa hadithi kutoka kwa ‘Uthman Ibn ‘Afan kuwa Mtume (s.a.w) amesema “mbora wenu ni yule mweye kujifunza quran kisha akaifanyia kazi” (Bukhari).

3. Mwenye kusoma quran hupandishwa daraja na Allah huwashusha daraja wasiosoma quran
Mtume (s.a.w) amesema “hakika Allah hupandihs (darja) watu kwa hii quran na kushusha (darja) watu kwa hii quran” (Muslim)  

عن عمرَ بن الخطابِ رضي اللَّه عنهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » إِنَّ اللَّه يرفَعُ بِهذَا الكتاب أَقواماً ويضَعُ بِهِ آخَرين « رواه مسلم

4. Allah humlipa msomaji wa quran kwa kila herufi moja atakayoisoma
عن ابن مسعودٍ رضيَ اللَّه عنهُ قالَ : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : منْ قرأَ حرْفاً مِنْ آتاب اللَّهِ فلَهُ حسنَةٌ ، والحسنَةُ بِعشرِ أَمثَالِهَا لا أَقول : الم حَرفٌ ، وَلكِن : أَلِفٌ حرْف،ٌ ولامٌ حرْفٌ ، ومِيَمٌ حرْفٌ « رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح
Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn Mas’ud kuwa Mtume (s.a.w) amesema “mwenye kusoma herufi moja (katika quran) Allah atampa jema. Na jema mojqa hulipwa mara 10….

5. Mtu ambaye hakuhifadhi chochote katika quran kwenye moyo wake ni sawa na jumba bovu
عنِ ابنِ عباسٍ رضيَ اللَّه عنهما قال : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : »إنَّ الَّذي لَيس في جَوْفِهِ شَيْءٌ مِنَ القُرآنِ آالبيتِ الخَرِبِ « رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح
Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn ‘Abas (r.a) kuwa amesema: Amesema Mtume (s.a.w) kuwa: “hakika yule ambaye hakuna katika kifua chake  (yaani hakuhifadhi) chochote katika quran ni sawa na jumba bovu”. (Tirmidh)

MWISHO
Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwakumbusha nduguzangu waislamu juu ya kuisahau quran baada ya kuihifadhi. Ndugu yangu Muislamu kati usiiwache quran uliyokwisha ihifadhi ikapotea kifuani kwako. Mtume (s.a.w) amekataza vikali sana kuhusu kuisahau quran. Darsa lijalo tutaangalia makatazo hayo.

Tafadhali tuunge mkono kwa kushea makala hii kwa wengine kwa ajili ya Allah.