Jumatano, 29 Machi 2017

IJUWE HISTORIA FUPI YA NABII LUT (A.S) NA WATU WAKE

                                      NABII LUT(A.S) NA WATU WAKE
                 


            NABII LUT (A.S)
Mtume Lut(a.s) ni mpwawe Ibrahiim(a.s) waliohama pamoja
yeye kutokea Iraq. Lut(a.s) alitumwa kuulingania Uislamu katika
miji miwili ya Sodoma na Gomora katika nchi ya Transjodan.
            TABIA YA WATU HAWA
Tabia ya Watu wa Miji ya Sodoma na Gomora
Jamii aliyoikuta Mtume Lut(a.s) ilikuwa imeanguka sana
kimaadili. Walifikia hali ya kuwa waovu zaidi ya wanyama licha ya
kuwa maumbile yao yalikuwa ya binaadamu. Walizama kwenye
kufanya maovu matatu mazito kama yanavyotajwa katika Qur-an:
Na (wakumbushe Nabii) Lut; alipowaambia watu wake: “Bila
shaka nyinyi mnafanya uovu (ambao) hakuna yoyote
aliyekutangulieni kwa (uovu) huo katika walimwengu.(29:28)

“Je, mnawaendea wanaume, na mnawakatia njia (watu kwa
kuwaua na kuwanyang’anya njiani) na mnafanya maovu katika
mikusanyiko yenu?” basi halikuwa jawabu ya watu wake ila
kusema: “Tuletee adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa umiongoni
mwa wasemao kweli!” (29:29)”
Katika aya hizi tunafahamishwa kuwa watu wa jamii ya Lut (a.s)
walikuwa wakifanya maovu mazito yafuatayo:
1) Walikuwa wakiwaendea wanaume wenzao katika
kutosheleza matamanio yao ya ngono.
2) Walikuwa wakifanya uharamia na uporaji wa mali za watu.
3) Walikuwa wakifanya maovu haya hadharani na kwa
ufahari.
Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao
(wa maovu); wanahangaika ovyo. (15:72)
Je, jamii yetu hivi leo haifanyi haya na zaidi ya haya tena kwa
ufahari. Hivi leo kuna mashindano ya U-miss ambayo wasichana
vigoli hujitokeza jukwaani mbele ya hadhara ya watazamaji
wanaume kwa wanawake wakiwa wamevaa viguo visivyo sitiri
mwili. Hali ni hiyo hiyo kwenye kumbi za dansi, disko na hata
kwenye sherehe za kiserikali. Na wengine wameenda mbele zaidi
hata kufikia wanawake kusoma taarifa za habari katika television
wakiwa uchi wa mnyama na kufikia wengine kucheza sinema za
wanawake na wanaume wakifanya ngono hadharani.
 Leo hii baadhi ya nchi za magharibi zimepitisha sheria yakuruhusu ndoa
baina ya wanaume kwa wanaume wakifanya ushenzi ule ule wa
mabaradhuli wa miji ya Sodoma na Gomora.
            NASAHA ZA NABII LUT(A.S)
Nasaha za Lut(a.s) kwa Watu Wake
Nabii Lut(a.s), kama Mitume wengine walivyofanya aliwanasihi
watu wake wamuamini Allah(s.w) na wamche ipasavyo na
waogope adhabu yake ambayo ikimfika mtu hapana awezaye
kuizuia au kuiondosha.
(Wakumbushe) alipowaambia ndugu yao, (Nabii) Lut: “Je,
hamuogopi?” “Bila shaka mimi kwenu ni Mtume muaminifu.”
“Basi Mcheni Mwenyezi Mungu na nitiini.(26:161-163)
“Wala sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa
(Mwenyezi Mungu) Mola wa walimwengu wote.” “Je,
mnawaingilia wanaume katika viumbe (vyake Mwenyezi
Mungu)!” “Na mnawacha alichokuumbieni Mola wenu katika
wake zenu? Kweli nyinyi ni watu mnaoruka mipaka
(mliyowekewa).”(26:164-166)
Na (wakumbushe) Lut alipowambia watu wake: “Je, mnaufanya
uchafu, na hali mnaona?” Mnawaingilia wanaume kwa

matamanio mabaya badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni
watu mfanyao ya ujinga kabisa. (27:54-55)
Pamoja na nasaha hizi nzuri zilizoambatana na hoja madhubuti,
hawakumuamini Lut(a.s) ila watu wachache tu.
Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu. (51:36)
Jawabu la Makafiri Dhidi ya Nasaha za Nabii Lut(a.s)
Pamoja na Nabii Lut(a.s) kuwanasihi kwa maneno ya hekima na
hoja zilizo wazi, watu wake hawakuwa tayari kabisa kuacha maovu
yale.
Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao
(wa maovu); wanahangaika ovyo. (15:72)
Walishakuwa walevi wa machafu hayo na walipania kumfukuza
Nabii Lut na wale walioamini pamoja naye ambao huchukia
ubaladhuli huo.
“Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila kusema: Wafukuzeni
wafuasi wa Lut katika mji wenu, hao ni watu wanaojitakasa,
(basi wasikae na sisi wachafu)” (27:56)
“Wakasema: Kama usipoacha, ee Lut (kutukataza haya), bila
shaka utakuwa miongoni mwa wanaofukuzwa (katika nchi hii).”
(26:167)

       KUANGAMIZWA KWA WATU WA NUHU (A.S)
Watu wa Lut(a.s) walipokataa kabisa kuonyeka kwa nasaha na
maonyo ya Nabii Lut(a.s) na badala yake wakazidi kushabikia
machafu na kupania kuwafanyia ubaya waumini, Allah(s.w)
alipitisha hukumu yake ya kuwanusuru waumini na kuwaangamiza
makafiri.
(Wale wajumbe) wakasema: “Ewe Lut! Sisi ni wajumbe wa
Mola wako (Malaika). Hawatakufikia (kwa baya lolote). Na
ondoka pamoja na watu wako katika sehemu ya pingapinga la
usiku.Wala yoyote miongoni mwenu asitazame nyuma.
Isipokuwa mke wako (mwanamke mbaya huyo hatakufuata).
Naye utampata msiba utakaowapata hao. Hakika miadi yao ni
asubuhi. Jee, asubuhi si karibu tu? (Basi tuliza moyo wako.
Umekwishafika wakatiwao wa kuangamizwa).(11:81)
Basi ilipofika amri yetu, tulifanya (ardhi hiyo iwe juu chini); juu
yake kuwa chini yake, na tukawateremshia mvua ya changarawe
za udongo mgumu (wa motoni uliyokamatana). (11:82)
(Changarawe) zilizotiwa alama kwa Mola wako (kila moja kuwa
ya mtu fulani). Na (adhabu) hii haiko mbali na madhalimu
(wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu
haya). (11:83)

Jeshi la Allah lililotumika kuwaangamiza watu wa Lut(a.s) ni
mvua ya changarawe kutokea motoni na kisha ardhi ikapinduliwa
juu – chini.
Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. (48:7)
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)
      MAFUNDISHO YATOKANAYO NA HISTORIA HII
Kutokana na historia ya Nabii Lut(a.s) tunajifunza yafuatayo:
(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika
jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama
alivyofanya Nabii Lut(a.s) na waumini aliokuwa nao.
(ii) Tusichelee watu katika kukemea maovu.
(iii) Kila mtu atahesabiwa na kulipwa kulingana na amali zake.
Hatafaidika mtu kwa amali njema za mwingine na wala
hataadhibiwa mtu kwa matendo mabaya ya mwingine.
(iv) Tumuogope Allah(s.w), kwani adhabu yake ni kali na hakuna
awezaye kujinusuru nayo inapokuja.
(v) Tujitahidi kusimamaisha Uislamu kwa mali na nafsi zetu bila
ya kumchelea yeyote.
(vi) Hatma ya mapambano dhidi ya makafiri ni Waislamu

kuibuka washindi.