Jumapili, 2 Aprili 2017

JIFUNZE KUPIKA KISAMVU , KABICHI, MAJANI YA MAMUNG'UNYAMBOGA YA KISAMVU


Kisamvu fungu 1 kubwa

Nazi 3

Vitunguu ¼  kilo

Chumvi kiasi

1                    Kichambue kisamvu ukikatekate ukipike mpaka kilainike.

2                    Kuna nazi  uchuje tui zito zito. Kata vitunguu vyembamba vyembamba.

3                    Maji yakishakauka tia vitunguu utie na tui upike mpaka tui likauke. kisha epua.MBOGA YA KABICHIKabichi kilo 1

Vitunguu ½ kilo

Samli ¼ kilo

Mayai 4

Tungule ¼  kilo

Pilipili manga kiasi

Chumvi kiasi

1                    Likate kate kabichi ulioshe ulpike mpaka liive.

2                    Kata vitunguu, katakata tungule na zisage pilipili manga.

3                    Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange. Tia tungule ukaange, tia kabichi, tia chumvi na pilipili manga. Kisha vunja mayai uyapige utie. Koroga mpaka likauke. kisha epuaMBOGA YA MAGANDA YA MAMUNG’UNYAMaganda ya mamung’unya kiasi

Vitunguu ¼ kilo

Tungule ¼ kilo

Mayai 4

Samli kiasi

Chumvi kiasi

Pilipili manga kiasi

1                    Yakate kate maganda ya mamungunya madogo madogo kama vitunguu, uyapikekwa maji mpaka yaive.

2                    Kata vitunguu, ukatekate tungule na usage pilipili manga.

3                    Teleka sufuria utie samli, ikichemka tia vitunguu uvikaange. Tia tungule ukaange, kisha yatie maganda pamoja na chumvi na pilipili manga. Vunja mayai uyapige uyatie. Koroga kidogo, ikikauka epua.

MCHUZI WA SAMAKISamaki kilo 1 (vizuri akiwa nguru)

Vitunguu maji ½ kilo

Nyanya ½ kilo

Vitunguu thomu kiasi

Samli ¼ kilo

Mbatata ½ kilo

Mdalasini kiasi

Pilipili mbichi kiasi

Bizari nzima kiasi

Hiliki kiasi

1        Mkate samaki umwoshe. Mtie chumvi na ndimu mkaange.

2        Kata vitunguu saga tungule, saga vitunguu thomu pamoja na viungo vyote vilivyobakia. Chemsha mbatata uzimenye.


3        Teleka sufuria utie samli. Ikichemka tia vitunguu maji uvikaange. Vikianza kupiga wekundu tia tungule. Kisha tia viungo vyote ulivyovisaga. Halafu tia mbatata na baadae utie vipande vyote vya samaki. Tia ndimu, chumvi na maji kidogo. Wacha vichemke kidogo. Onja ukiona kila kitu sawa, epua


       REFERENCE
click here