Alhamisi, 23 Machi 2017

IJUWE SWALA YA MAITI NA NAMNA YA KUISWALI

bofya hapa
                                       Kumswalia Maiti.

·         Masharti ya Swala ya Maiti.
-     Kwa wenye kumswalia maiti, watekeleze masharti ya kawaida ya swala.
-     Masharti ya maiti anayeswaliwa:
o   Maiti awe muislamu
o   Maiti iwe imeoshwa na kukafiniwa
o   Maiti iwekwe mbele ya wanaoisalia.
--  Inajuzu kusalia maiti iliyo masafa ya mbali (swala ya ghaibu).
-- Maiti zikiwa nyingi zipangwe mbele, za kiume zikiwa karibu
 na imamu kisha kusaliwa zote kwa pamoja.
o   Maiti isiwe ya shihidi.
                        -- Kwa mujibu ya Hadith ya Mtume (s.a.w), mashahidi hawaoshwi wala kusaliwa.    
·     

   


Nguzo za Swala ya maiti.
-     Swala ya maiti inaswaliwa wima; haina rukuu, sijda wala kikao.
-     Nguzo za swala ya maiti ni;
                                                        i.            Nia
                                                      ii.            Takbira ya kuhirimia
                                                    iii.            Kusoma Suratul-Faatiha.
                                                    iv.            Takbira ya Pili.
                                                      v.            Kumswalia Mtume (s.a.w) kama tufanyavyo kwenye Tahiyyatu.
                                                    vi.            Takbira ya Tatu.
                                                  vii.            Kumuombea dua maiti.
                                                viii.            Takbira ya Nne.
                                                    ix.            Kuombea dua waislamu wote, kisha kutoa Salaam.

·        pata Darsa mbalimbali za Quran
      bila ya kuhitaji internet. Bofya hapaNamna ya kutekeleza swala ya Maiti hatua kwa hatua.
Utaratibu wa kusimamisha swala ya maiti ni kama ifuatavyo;
a)      Maiti iwekwe mbele.
b)  Imamu asimame katikati ya mwili wa maiti ikiwa maiti ni ya kike, na usawa wa mabega kama maiti ni ya kiume.
c)      Maamuma watasimama kwenye mistari (safu) kwa idadi ya witiri; 1, 3, 5, n.k.
d)     Baada ya hapo swala itaanza na kuendelea kama ifuatavyo:
                                 i.            Nia - ambayo ni kukusudia moyoni.
                             ii.            Kuleta takbira ya kwanza; kwa kusema, “Allaah Akbar”
                             iii.            Imamu na maamuma watasoma suratul-Faatiha – kimya kimya.
                   iv.            Imamu ataleta Takbira ya Pili kisha maamuma – kimya kimya kwa maamuma na si lazima kuinua mikono wao.
                               v.            Kumswalia Mtume (s.a.w) kama ilivyo katika Tahiyyatu, wote – kimya kimya.
                            vi.            Imamu ataleta takbira ya Tatu kisha maamuma- kama walivyofanya awali.
   vii. Wote kumuombea maiti dua kimya kimya, ikiwemo:“Allaahumma ghfirlihayyinaawamaayyitinaa washaahidinaa waghaaibinaa waswaaghirinaa wakaabirinaa wadhakirna waunthaanaa. Allaahumma manahyaytahuuminnaa faahyi ‘alal Islaam. Waman tawaffaytahuu minnaa tawaffahuu ‘alal Imaani. Allaahumma laa tahirimnaa ajirahuu walaa taftinaaba’adahuu”
            Tafsiri:
“Ewe Allah tusamehe sisi, na maiti wetu, na mashahidi, na wasiokuwepo miongoni wetu, vijana wadogo miongoni mwetu na wakubwa miongoni mwetu, wanamume wetu, na wanawake wetu. Ewe Allah, yeyote yule miongoni mwetu utakayemewezesha kuishi, mjaalie aishi katika Kiislamu na yeyote miongoni mwetu utakayemfisha, mfishe katika Imani (ya Kiislamu). Ewe Allah, usitukatishe ujira kutoka kwake na wala usitufitinishe baada yake.”

                        -   Au kwa kifupi tuweza kumuombea maiti kama ifuatavyo;
                                    “Allaahumma ghfir lahuu warhamhuu wa-afihii wa-afu-anhu”
                        Tafsiri:
                                    “Ewe Allah, Mghufirilie na Umrehemu”.


Jifunze namna ya kuswali, bila ya kuhitaji internet
ukiwa na App yetu, bofya hapa

                                                viii.            Imamu ataleta Takbira ya nne na maamuma kufuatihia kama awali.
                                                    ix.            Wote watawaombea waislamu dua – (pia si lazima kuleta dua hii).
Rejea Qur’an (59:10).

                                                      x.            Imamu kutoa salaam na maamuma kufuatishia bila kutoa sauti kama ilivyo kwenye swala ya kawaida kwa kusema;
                  “Assalaamu ‘alaykum Warahmatullaah (Wabarakaatuh)”
      Tafsiri:
                  “Amani iwe juu yenu na Rehema za Allah na Baraka zake”.

  Usiwache kuwa nasi katika post zetu nyingine 
>>> Kupata update zetu fuata link zifuatazo.<<<
>>> Bofya hapa kupata yanayojiri katika blog hii

>>> Bofya hapa kuungana nasi youtube ili upate video zetu nyingine

>>> Bofya hapa kupata masomo zaidi ya afya ukiwa na app yetu

>>> Ungana nami kwenye FACEBOOK

VIDEO MUHIMU KUANGALIA
>>>>1.Dhambi kubwa<<<<<<
>>>2.miujiza ya quran<<<<<<<
>>>3.Pambana na maradhi na dhibiti afya yako<<<<<<

>>> CLICK HERE <<>>>>>