Jumapili, 16 Julai 2017

ZIJUE AINA ZA TALAKA, HUKUMU ZAKE, NA TARATIBU ZA KUTALIKI KATIKA UISLAMUAsalaamu alykum warahmatuLah wabarakaatuh.
sifa njema zinamsatahikia Allah mola wa ulimwengu. Rehma na amani zimfikie Kipenzi cha Allah Mtume wetu Muhammad (s.a.w). ama baada ya utangulizi huo mfupi, hii ni katika mfululizo wa darsa zetu za kifiqh. unaweza kupata darsa nyingine ukiwa na program zetu kwenye simu yako ya kiganja. bofya hapa kuapata program zetu. au bofya hapa kusoma darsa mbalimbali za dini.
Aina za Talaka
Kuna aina kuu mbili za talaka
a) Talaka rejea
b) Talaka isiyo rejewa

a) Aina za Talaka Rejea
- Ni aina ya talaka inayompa mume fursa ya kumrejea mkewe baada ya kumpa talaka katika kipindi cha twahara.
i. Talaka moja
Ni aina ya talaka ambapo mume humtamkia au kumuandikia mkewe “nimekuacha” kwa talaka moja akiwa twahara.

ii. Talaka mbili
Ni aina ya talaka ambapo mume humuacha mara ya pili baada ya kumuacha kwa talaka moja kisha akamrejea katika twahara mbili tofauti.
Rejea Qur’an (2:229)

iii. Talaka ya ‘Ilaa
Ni aina ya talaka ambapo mume humtenga mkewe kwa zaidi ya miezi mine.
Rejea Qur’an (2:226)
iv. Talaka ya Zihaar
Ni aina ya talaka ambapo mume humsusa mkewe kwa kumfananisha na mama yake mzazi au maharim wake.
Kama hatatubia kabla ya kuisha miezi minne, mkewe atakuwa ameachika.
Rejea Qur’an (58:3-4)

 Jifunze swala na adhkar mbalimbali
ukiwa na App yetu bila ya internet. bofya hapa


v. Talaka ya Khul’u
Hii hupatikana kwa mke kudai talaka au kujivua katika ndoa kutokana na makubaliano tangu mwanzo katika mkataba wa ndoa.
Mke anayedai talaka, atalazimika kumrejeshea mume mahari aliyompa ili ajikomboe.
Rejea Qur’an (2:229)

vi. Talaka ya Mubaarat
Ni aina ya talaka ambapo mume na mke hukubaliana kuachana kwa wema baada ya kutofikia lengo la ndoa.

vii. Talaka kabla ya Jimai
Ni kuvunja mkataba wa ndoa kabla ya kufanya tendo la jimai (ndoa).
Talaka hii ina taratibu zifuatazo;
- Hapana kukaa eda kwa mwanamke aliyeachwa kabla ya tendoa la jimai.
- Kama mume ndiye aliyemuacha na ameshatoa mahari, hatadai chochote.
Uk. 58 kati ya 1 3 1
- Mume atalazimika kumpa mkewe kitoka nyumba kama ndiye aliyeamua kumuacha.
- Ikiwa mume alikuwa hajatoa mahari, atalazimika kutoa nusu ya mahari.
- Kama mke ndiye aliyedai talaka atamrudishia mumewe mahari aliyompa
Rejea Qur’an (2:236-237)


Kitabu cha Afya
 Bofya hapa

b) Aina ya Talaka Zisizorejewa
- Ni aina ya isiyompa mume fursa ya kumrejea mkewe baada ya kumuacha kwa talaka mbili ila mpaka aolewe na mume mwingine kisha aachike kisheria.
i. Talaka tatu (Tahliil)
Ni talaka ambayo mume humuacha mkewe baada ya kumrejea kutoka talaka mbili alizomuacha na kumrejea hapo awali.
Rejea Qur’an (2:230), (65:1)

ii. Talaka ya Li’aan
Ni talaka inayopatikana baada ya mume au mke kumshika ugoni mwenzake bila ya kuwa na mashahidi wanne.
Kila mmoja ataishuhudilia nafsi yake kwa kula kiapo mara tano mbele ya kadhi na baada ya hapo ndoa itavunjika na kutorejeana tena.
Rejea Qur’an (24:6-9)

Soma hadithi za Alif lela u lela
Bila ya kuhitaji internet ikiwa na pp yetu Taratibu na Sharti za Kutaliki Kiislamu
i. Talaka hutolewa kwa matamshi au maandishi kuwa “nimekuacha” au maneno yenye maana mfano wake.
ii. Talaka itamkwe au itolewe mke akiwa katika kipindi cha twahara na wasiwe wamefanywa tendo la ndoa ndani ya twahara hiyo.

iii. Utoaji wa talaka ni vema ushuhudiwe na mashahidi wawili waadilifu.


iv. Mke aliyetalikiwa hukaa nyumbani kwa mumewe mpaka eda iishe ambapo hutengana tu kimalazi.

v. Kama mume na mke wataamua kurejeana kabla ya eda kwisha, watarejeana kwa wema kwa kumuahidi Allah (s.w) kuwa wataishi kwa wema.

vi. Baada ya eda kwisha, mume na mke watalazimika kuachana kwa wema kama anavyoamrisha Allah (s.w).

vii. Si halali kwa mume aliyetoa talaka kuchukua au kudai chochote katika vile alivyompa mkewe.

viii. Mume aliyemuacha mkewe, analazimika kumpa mtaliki wake kitoka nyumba.
Rejea Qur’an (2:236)

ix. Mke aliyeomba talaka anawajibika kujikomboa kwa kumrudishia mtalaka wake mahari aliyompa, na mume akisamehe hapana ubaya                  POST MUHIMU KWA AJILI YAKO
       >>> FAHAMU UGONJWA WA SARATANI
       >>>> NAMNA YA KUONDOWA VIRUSI KWENYE SIMU
       >>>> NJIA RAHISI YA KUPAMBANA NA MAFUA