MCHUZI WA UBONGO
Ubongo kilo
1
Vitunguu ½
kilo
Tungule ½
kilo
Samli ¼ kilo
Thomu kiasi
Bizari nzima
kiasi
Hiliki kiasi
Pilipili
manga kiasi
Mdalasini
kiasi
Chumvi kiasi
Tangawizi
mbichi kiasi
1 Uoshe ubongo upachuepachue
uweke katika chujio uvuje maji.
2 Kata vitunguu, saga thomu,
tungule pamoja na viungo vyote vilivyobakia.
3 Teleka sufuria utie
samli.Ikichemka tia vitunguu uvikaange mpaka vipige wekundu. Tia tungule
ukaange. Kisha tia viungo vyote ulivyovisaga. Mwisho tia ubongo ukaange. Baadae
tia chumvi, limau na maji kidogo. Acha uchemke, ukikauka epua.
REFERENCE
click here