Jumanne, 21 Machi 2017

KWA NINI LENGO LA SWALA HALIFIKIWA NA WENGI WANAOSWALI?

                KWA NINI LENGO LA SWALA HALIFIKIWI?


§  Kwa nini Wengi wanaoswali hawafikii Lengo la Swala zao?
    Kama tulivyoona lengo la swala katika post zilizopita bofya hapa kusoma post hiyo. Sasa hebu leo tuone kwa nini lengo la swala halifikiwi na wengi wanaoswali?
Miongoni mwa sababu ya wengi kutofikia malengo ya swala zao ingawa wanaziswali misikitini tena kwa jamaa ni;

1.      Hawajui lengo halisi la swala.
Waislamu wengi huswali kwa lengo la kufutiwa madhambi na kupata thawabu na sio kuepukana na machafu na maovu, ambalo ndio lengo kuu la swala. Kupata thawabu na kufutiwa madhambi ni matunda ya swala.
Rejea Qur’an (29:45) na (72:23).

2.      Waislamu wengi hawana ujuzi sahihi juu ya swala.
Pamoja na waislamu wengi kutekeleza swala zao kwa jamaa lakini wengi wao hawajui kabisa miiko, sharti na nguzo za swala ila wanafuata mkumbo tu.
Rejea Qur’an (7:205), (7:55) na (4:142).

3.      Waislamu wengi hawahifadhi swala zao.
Pamoja na kuswali kwao bado wengi hawazingatii na kutekeleza kikamilifu sharti na nguzo za swala zao inavyotakiwa.
Rejea Qur’an (107:4-5) na (23:1,8).

4.      Wengi hawaswali kwa Unyenyekevu swala zao.
Kukosa unyenyekevu (utulivu wa mwili, fikra na uzingativu) hupelekea mwenye kuswali kutofikia lengo na matunda ya swala.
Rejea Qur’an (29:45), (23:1-2) na (23:10-11).

5.      Kutosimamisha Swala za jamaa ipasavyo.
Waislamu wengi hawaswali jamaa misikitini au hawazingatia sharti za swala ya jamaa kama kunyoosha safu ipasavyo, kugusanisha mabega, vidole, n.k.
Rejea Qur’an (23:1-2).