Kuoshwa kwa MAITI (Kukoshwa).
·
Mazingatio
kabla ya kuosha maiti.
(a)
Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike
ioshwe na wanawake pia.
- Maiti ya mtoto
yaweza kuoshwa na yeyote.
- Ni Sunnah mke
kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe pia
(b)
Ni mtu mmoja tu ndiye anayeosha na mwingine ni kwa
ajili ya kumpa msaada inapobidi.
(c)
Ni muhimu muoshaji afahamu masharti ya kuosha maiti
muislamu kama vile;
o
Muoshaji awe muislamu.
o
Mahali pakuoshea pawe faragha (pamesitirika).
o
Maiti aoshwe huku amefunikwa gubi-gubi na nguo
nyepesi inayoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
o
Ni vyema muoshaji asiishike maiti bali aoshe
akiwa amevaa ‘gloves’.
o
Kuzingatia masharti ya mwenye kuoga josho la
wajibu; kama vile kuwa na maji mengi na safi ,
pasiwe na kizuizi cha maji kupenya, n.k.
(d)
Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na sunnah za kuosha
maiti kama ifuatavyo;
- Nguzo za kuosha maiti ni mbili:
o
Nia
o
Kueneza maji mwili mzima wa maiti.
- Ni Sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi
kwa idadi ya witiri.
§
Namna ya
Kuosha Maiti hatua kwa hatua.
i.
Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati ili
kupitisha uchafu unaotoka tumboni.
ii.
Pawepo na shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, kama hakuna uwekano chombo kiwepo cha kukingia uchafu
unaotoka kwa maiti.
- Pia maiti inaweza kuoshewa bafuni au kwenye
karo liliotengenezwa
kwa kazi hiyo.
iii.
Maiti afunikwe na nguo moja kubwa yenye kupenyeza maji
wakati wa kuosha.
iv.
Maiti akalishwe juu ya kitanda usawa wa tobo na shimo
(ufuo) na ainamishwe nyuma kidogo, kama ni
mzito ni vizuri msaidizi wa muoshaji amuegemeze kwenye magoti yake.
v.
Muoshaji apitishe mkono wa kushoto kwenye tumbo la
maiti na kuliminyaminya taratibu ili kutoa uchafu ndani.
vi.
Amlaze chali na kuminyaminya tumbo lake kama
ilivyo mara ya kwanza.
vii.
Aikalishe tena na apitishe mkono wa kushoto chini akiwa
amevaa kitambaa au gloves na kusafisha tupu mbili kwa maji safi .
- Kama hapaja
takata, basi na avae gloves safi
na ile chafu aitupe kwenye
ufuo na asafishe tena kama mara ya
kwanza mpaka patakate.
viii.
Baada ya hapo, muoshaji afunge kitambaa safi kwenye kidole chake
shahada na akichovye kwenye maji na kumswakisha maiti meno yote na kisha
akitupe ufuoni.
ix.
Muoshaji azungushe kitambaa kingine safi kidole chake kidogo mkono wa kushoto na
kumsafisha nacho maiti tundu za pua kisha akitupe ufuoni.
x.
Asafishe kucha za maiti kwa kijiti safi na laini iwapo ni ndefu na chafu.
xi.
Kisha amkalishe maiti na amtawadhishe kwa kufuata taratibu
za kawaida za kutia udhu (kutawadha).
xii.
Maiti akiwa amekalishwa, ataanza kumuoshwa kichwa akiwa
ameinamishwa mbele kidogo.
- Kama nywele au ndevu
ni nyingi zichanwe na kuoshwa kwa sabuni na
maji mpaka
zitakate.
-
Mwanamke mwenye nywele nyingi zisukwe mikia, na zilizong’oka
ziambatanishwe na sanda.
xiii.
Baada ya kuoshwa kichwa, maiti italazwa kwa ubavu wa
kushoto na kuanza kuoshwa ubavu wa kulia, mbele na nyuma kwa pamoja kwa sabuni
na maji safi mpaka itakate.
xiv.
Kisha itaoshwa ubavu wa kushoto kama
ilivyooshwa wa kulia.
xv.
Baada ya makosho (maosho) haya mawili, la maji na
sabuni na la kuondoa sabuni, kosho la tatu la maji liwekewe karafuu na marashi
ili kulegeza viungo (maungo) vya maiti.
xvi.
Baada ya makosho matatu haya, muoshaji anyooshe viungo
vya maiti na kumlaza kama alikuwa mara tu
baada ya kufa.
xvii.
Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti, na baada ya
hapo maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na kufunikwa kwa nguo kavu tayari
kuvalishwa sanda (kukafiniwa).