Ijumaa, 21 Aprili 2017

IJUWE MAANA YA KUAMINI MALAIKA NA KAZI ZAO.

Asalaamu 'alaykum
       Sifanjema zinastahiki kusifiwa Allah Mola wa ulimwengu. Salana Salamu zimuendee kipenzi cha umma huu Mtume Muhammah (s.a.w). huu ni mwendelezo wa Darsa zetu mbalimbali ambapo tutajifunza Kuhusu Kuamini malaika. Tunamuomba Allah atupe Afya na uzima katika kulitekeleza hili. Pia unaweza kuzipata Darsa hizi bila ya kuhitajia intanet ukiwa na program yetu ya simu (Android App). unaweza kuidaunload kwa kubofya hapa. Unaweza pia kusoma darsa nyenginezo kwa kubofya link zifuatazo;-
1.Darsa za funga bofya hapa
2.Darsa za Dua bofya hapa
3.Mafunzo ya tajwid (kusoma quran) bofya hapa
4.Quran Juzuu 'Amma bofya hapa



             Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).
         Maana: Malaika ni viumbe walioumbwa kutokana na nuru.

        Sifa za Malaika:
- Ni viumbe wa kiroho wenye mabawa.
- Ni viumbe wasio na matashi ya kimwili (kula, kunywa, kulala, n.k.)
- Hawana hiari katika kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w).
- Ni vimbe wasio na jinsia.
- Ni viumbe walioumbwa kutokana na Nuru.




                        tazama video hii 
         
                                                        

                                             Kazi za Malaika.
                     Zifuatazo ni baadhi tu ya kazi za baadhi ya Malaika.
(a)    Kuleta Wahyi (ujumbe) kwa wanaadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Malaika Jibril ndiye mhusika mkuu wa kupeleka wahyi kwa mitume na manabii.
Rejea Qur’an (81:19-20), (16:2) na (11:69-73).

(b)    Kumchunga na Kumlinda kila mtu na kuandika amali zake nzuri na mbaya.
Kila mtu anakundi la malaika nyuma na mbele yake kumlinda na mambo yaliyo nje na uwezo wake. Pia kuna malaika wa kulia anayeandika mema na wa kushoto anayeandika maovu ya mtu.
Rejea Qur’an (82:1-12), (50:17-18) na (13:11).

(c)     Kuwaombea Waumini maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Hawa ni malaika ambao huzunguka katika makundi ya waumini anapotajwa ndani yake Mwenyezi Mungu (s.w) au kusomwa Qur’an Tukufu.
Rejea Qur’an (40:7), (42:5) na (17:78).

(d)    Kuwasaidia waumini katika vita vya kupambana na maadui wa Allah (s.w).
Pindi waumini wanapopigana katika kusimamisha haki, Mwenyezi Mungu (s.w) huteremsha malaika kuwasaidia.
Rejea Qur’an (3:123-126) na (8:12).

Jifunze swala ukiwa na app yetu
Bofya hapa




(e)     Kuwaangamiza watu waovu waliopindukia mipaka.
Watu waovu waliopindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) wakaonywa muda mrefu na wasionyeke huangamizwa na malaika maalum.
Rejea Qur’an (11:81-83).

(f)      Kutoa roho za viumbe.
Malakul-Maut ndiye mhusika mkuu na wengineo katika kutoa roho za viumbe.
Rejea Qur’an (32:11).

(g)    Kuzihoji, kuzistarehesha au kuziadhibu roho za wafu kaburini.
Malaika wanaohusika na kazi hii ni Munkar na Nakir.

(h)    Kupuliza Parapanda siku ya Qiyama.
Mipulizo ya Parapanda katika kufisha na kufufua viumbe siku ya Qiyama itafanywa na malaika Israfil.
Rejea Qur’an (39:68).

(i)      Kuwaliwaza na kuwakaribisha watu wema peponi.
Hili kundi jingine la malaika watakaofanya kazi hiyo siku ya Qiyama.
Rejea Qur’an (41:30-32) na (39:73).

(j)      Kuwasimanga na kuwaadhibu watu waovu motoni.
Kuna kundi la malaika watakaokuwa wanaadhibu watu waovu motoni. Mlinzi mkuu wa milango ya moto ni Malaika Maalik.
Rejea Qur’an (25:22), (74:26-30) na (43:77).

(k)    Kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu (s.w).
Kuna kundi la malaika maalum kwa kazi hii tu.

  



Maana ya Kuamini Malaika katika maisha ya kila siku.
Zifuatazo ni athari za muumini wa kweli juu ya imani ya malaika katika kila kipengele cha maisha ya kila siku;

Kwanza, imani ya kweli juu ya Malaika humuepusha na kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w) na viumbe wake hasa wale wasioonekana kama Malaika, majini, n.k.
Rejea Qur’an (37:149-154), (43:16-19) na (21:26-27).

Pili, imani juu ya malaika huchochea mja kufanya ibada kwa bidii na kujiepusha na maovu na machafu ili kupata cheo kama malaika au zaidi.

Tatu, imani juu ya malaika pia humfanya mtu kuepuka kufanya maovu popote alipo na muda wowote kwa kujua kuwa yupo pamoja na malaika.

Nne, Mja anapoamini kuwa malaika huandika na kuhudhurisha vitendo vyake kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kufanya mema zaidi na kuepuka maovu kadri ya uwezo wake.


soma quran juzuu amma pamoja na audio zake
Bila ya kuhitaji internet ukiwa na App yetu



Tano, Muumini anapoamini kuwa malaika humuombea maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kuzidisha mema na kuepuka maovu kadri awezavyo ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu (s.w) zaidi.

Rejea Qur’an (17:13-14) na (18:49).