SAUMU YA FARDHI (Ramadhani)
Nini Saumu?
Saumu kilugha ni kujizuiya na kitu, yaani kutofanya kitu
fulani; kama ilivyo kwenye QurĂ¡ni Tukufu:
" .........
Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo
sitasema na mtu". (Maryam : 26).
Kisharia Saumu ni kujizuia kula, kunywa na matamanio ya
utupu; tangu alfajiri mpaka kutua jua pamoja na kutia nia ya hio saumu. Hivi
kutia nia ni kwa qauli ya Mtume s.a.w. kwa kukhusu kila ibada, yaani kutimia
ibada ni kuwepo na kutimia nia: Maana ya
Hadithi hii ni kama hivi:
"Hakika ya kila kitendo ni kwa nia yake".
Hukmu Yake
Saumu ni nguzo ya nne kati ya nguzo tano za Uislam.
Kulazimika saumu kumekuja kwa Qauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kufasiriwa
kwa qauli ya Mtume s.a.w. na wanazuoni wakawafiqiana juu ya hili. Amesema
Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo
andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu”. (Al Baqara : 183).
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
"..... Basi
ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge.....".(Al Baqara : 185).
Na Hadithi ya Mtume s.a.w.:
Maana ya Hadithi hii ni kama hivi: "Umejengwa Uislam juu ya (Nguzo)
tano".
Katika nguzo tano hizo, ikatajwa nguzo ya nne kuwa ni Saumu
ya mwezi wa Ramadhani. Mtu alimuomba Mtume s.a.w. amfahamishe saumu
alioifaridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake. Akasema Mtume s.a.w.: , yaani Saumu ya Mwezi wa Ramadhani".
Saumu imewajibikishwa juu ya Muislam, baalegh, mwenye akili
kaamili, mwenye uwezo wa kufunga. Saumu haimuwajibikii Kafiri wa asili, wala
haisihi juu yake Saumu, kwa vile yeye si mwenye kuhisabika kuwa ni katika wenye
kufanya ibada, vilevile Saumu haimuwajibikii mtoto mdogo. Saumu haimlazimikii
mtoto, lakini mtoto huzoeleshwa kufunga tangu udogoni. Vilevile Saumu
haimuwajibikii mgonjwa wa akili. Hivi ni kwa qauli ya Mtume s.a.w.:
Maana ya Hadithi hii ni kama hivi:
"Imeondoshwa kalamu (kulazimika na hukmu za Sharia) kwa
watu watatu: mwenye kulala mpaka aamke, mtoto mdogo mpaka abaleghe, na mgonjwa
wa akili mpaka apowe". (Imehadithiwa na Abu Daud).
Ama yule asieweza kufunga, au kama atafunga atapata madhara
ambayo hayatarajiwi, hivi ni kama vile mtumzima (mkubwa wa umri), au mtu mwenye
maradhi ambayo hayatarajiwi kupona, hawa haiwajibikii juu yao kufunga, lakini
itawalazimikia kafara. Kafara ya katika hali hii ni kutoa kibaba cha chakula
cha kawaida cha nchini kwa kila siku
anayoshindwa kufunga, ikiwa ni mwenye uwezo wa kufanya
hivyo, ikiwa
hana uwezo, baadae akapata uwezo itamlazim atekeleze kafara
hii ambayo ni dhima juu yake.
Fardhi za Saumu
Saumu ina fardhi tano:
Ya Kwanza, nia; na mahala pake ni moyoni; na ni waajibu
kutia nia kila usiku wa kuamkia (kabla ya alfajiri) siku ya saumu. Hivi ni kwa
qauli ya Mtume s.a.w.: "Asietia
nia (ya kufunga, Saumu ya fardhi) tangu kabla ya alfajiri basi hana
Saumu". (Imehadithiwa na Ahmad na wapokezi wa Hadithi).
Ya Pili na Tatu, kujizuia kula na/au kunywa hata chembe
ndogo tangu kuingia alfajiri mpaka kuingia magharibi. Kujizuia huku ni kwa
kujizuia na kila kitu kufika tumboni/ndani ya mwili kwa njia ya tundu za mwili
zilizo wazi, kujizuia huku kuwe kunakusudiwa khaasa kwa ajili ya kutekeleza hii
ibada ya saumu.
Ya Nne, kujizuia kuingilia utupu wowote ule na/au kujitoa
manii kwa njia yoyote ile, ikiwa kwa mkono au kwa kuchezeana. Haya ni kwa Qauli
ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"
.…..Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni
Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri
katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku.........". (Al
Baqara : 187).
Ikiwa mtu atatokezea akala au akanywa hali ya kuwa amesahau
kuwa ana saumu; Saumu yake haitaba'tilika; hivi ni kwa qauli ya Mtume s.a.w.:
"Mwenye kusahau
kuwa kafunga, akala au akanywa; basi naatimize Saumu yake kwani yeye amelishwa
na amenywishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu". (Imehadithiwa na Jama'a
Wapokezi Hadithi)
Vilevile kwa qauli ya Mtume s.a.w.:
"Hakika Mwenyezi
Mungu Mtukufu amewasamehe umati wangu kwa la kukosea na la kusahau na la
kulazimishwa". (Imehadithiwa na Ibnu Maajah na Al 'Tabrany na Al Haakim).
Ya Tano, kujizuia na kujitapisha. Ikiwa atatapika bila ya
kukusudia basi Saumu yake haitaba'tilika, hivi ni kwa qauli ya Mtume s.a.w.:
"Mwenye
kutapika (si makusudi) nae amefunga, haimlazim kuilipa Saumu yake, na mwenye
kujitapisha (makusudi) basi naailipe Saumu yake". (Imehadithiwa na
Wapokezi Hadithi).
MAREJEO