Alhamisi, 24 Agosti 2017

Fadhila Za Siku Ya 'Arafah Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja)

Fadhila Za Siku Ya 'Arafah Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja)

 ‘Arafah ni jabali ambalo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama katikati ya bonde lake kuhutubia Maswahaba katika Hajjatul-widaa’i. (hajj ya kuaga), na hapo ndipo wanaposimama Mahujaji kutimiza fardhi ya Hajj. Kusimama hapo ndio nguzo mojawapo kuu ya Hajj. Bila ya kusimama ‘Arafah hijjah ya mtu itakuwa haikutimia kwa dalili ifuatayo:

عن عبد الرحمن بن يعمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:  ((الْحَجُّ عَرَفَة، مَنْ جَاءَ قَبْلَ طُلُوعِ الْفَجْرِ مِنْ لَيْلَةِ جَمْعٍ فَقَدْ أَدْرَكَ الْحَجّ))  صحيح الجامع   
 ‘Abdur-Rahmaan bin Ya’mur (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Al-Hajj ni ‘Arafah, atakayekuja kabla kutoka Alfajiri usiku wa kujumuika atakuwa ameipata Hajj)) [Swahiyh Al-Jaami’].
  alhidaayah.com