HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU.
1. Dhana ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.
§
Maana ya
Haki kwa Mtazamo wa Uislamu.
Ni muunganiko
wa sheria na maadili kwa lengo na madhumuni ya kuilea jamii katika amani,
furaha, udugu wa kweli na mahusiano mema kati ya wanaadamu.
§
Misingi
ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.
Maisha ya
furaha na amani ya kweli hupatikana kwa kusimama misingi ya haki na Uadilifu
katika jamii kama ifuatavyo;
i.
Tawhiid.
Haki na
Uadilifu wa kweli hupatikana kwa kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w)
ipasavyo katika maamrisho na makatazo yake.
ii.
Utume.
Katika
kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) ni kufuata misingi ya miongozo ya
mitume wake wote kupitia vitabu vyao.
iii.
Siku ya Mwisho.
Kumpwekesha
Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha yetu ni kuzingatia kuwa kila kitendo
kitahukumiwa na kulipwa kwa haki siku ya Kiyama.
§
Aina au
migawanyo mbali mbali ya Haki katika Uislamu.
1.
Haki za Allah.
2.
Haki za Nafsi.
3.
Haki za Viumbe na Mazingira.
4.
Haki za Binadamu kwa ujumla.
5.
Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu.
6.
Haki za Maadui katika Vita (mateka).
1. Haki za Mwenyezi Mungu (s.w).
Katika Uislamu haki za Mwenyezi Mungu ziko makundi mawili;
i.
Haki ya
Uungu.
Ni kumsifu na
kumtii kwa sifa zake kama za uumbaji,
umilikaji na ulezi wa viumbe vyote na ukamilifu wake tofauti na viumbe
alivyoviumba.
Rejea Qur’an (45:23), (25:68), (9:31) na (31:13).
ii.
Haki ya
Kuabudiwa.
Ni Mwenyezi
Mungu (s.w) peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa na viumbe vyake muda wote,
na ndio lengo kuu la kuumbwa mwanaadamu.
Rejea Qur’an (51:56), (5:44), (11:25-26) na (29:16-17).
2. Haki za Nafsi.
Haki za nafsi imekokotezwa kuanzia binafsi, familia, wazazi, n.k kama ifuatavyo;
(a)
Mtu Binafsi.
Haki za msingi
ni chakula, makazi, malezi, elimu, mavazi, matibabu na kufanyia kazi vipaji na
neema alizonazo inavyostahiki ikiwemo;
·
Haki ya
Macho.
Ni kutazama yaliyoamrishwa na kuyaepusha na yaliyoharamishwa.
Rejea Qur’an (17:36), (41:20),
(24:30-31) na (20:131).
·
Haki ya
Masikio.
Ni kusikiliza yaliyoamrishwa na kutosikiliza yaliyoharamishwa pia.
Rejea Qur’an (8:22) na (6:25).
·
Haki ya
Midomo na Ulimi.
Ni kula, kunywa na kuzungumza yaliyohalalishwa na sio yaliyoharamu.
Rejea Qur’an (16:114), (17:26-29), (17:53), (41:33) na (31:6).
·
Haki ya
Mikono na Miguu.
Ni kushika na kuendea vyote vilivyoamrishwa na kuacha vilivyokatazwa.
Rejea Qur’an (25:72) na (31:18).
(b) Haki za Familia.
Ni
kusimamia malezi, elimu, uadilifu na wajibu wa kila mmoja katika familia kwa muongozo wa Qur’an na Sunnah ili kuleta
kufikia lengo la kuumbwa.
Rejea Qur’an
(52:21).
(c) Haki za Watoto.
Watoto
wana haki ya kupata malezi na makuzi bora kulingana na mahitaji yao kwa mujibu wa
mafundisho ya Qur’an na Sunnah katika sehemu zifuatazo;
·
Haki ya
Uhai.
Uhai
wa mtoto ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kupitia malezi na makuzi ya
wazazi.
·
Haki ya
Nasaba.
Mtoto kupata
nasaba ni haki kisheria ili kuwa mwanafamilia halali.
Rejea Qur’an
(33:4).
·
Haki ya Makuzi
na Malezi bora.
Makuzi
na malezi bora ya mtoto ni kupata haki zake za msingi na elimu inayomuwezesha
kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo.
Rejea Qur’an
(66:6).
(d) Haki za Wazazi.
Ni
kuwahurumia, kuwaheshimu, kuwafanyia wema, kuwahudumia na kuwalea ipasavyo.
Rejea Qur’an
(31:14), (17:23-24), (4:36), (6:151), (19:14) na (19:32).
(e) Haki za Jamaa na Majirani.
Ni kutunza
uhusiano na kusaidiana pale inapohitajika kwa kuzingatia mipaka.
Rejea Qur’an
(2:215).
(f) Haki za Mayatima, Wajane na Masikini.
Ni kuwahifadhi na
kuwasaidia wanapokuwa na shida na mahitaji ya kimaisha.
Rejea Qur’an
(2:220), (4:2), (4:10), (2:262) na (2:267).
(g) Haki za Udugu wa Kiimani na za Watu wengine.
Udugu wa kiimani
ni haki na bora zaidi kuliko udugu wa damu au nasaba.
Rejea Qur’an
(49:10), (49:13), (7:172-173), (4:7) na (5:8).
3. Haki za Viumbe na Mazingira.
Uislamu
umeweka kipaumbele katika kuhifadhi mazingira na kutunza viumbe hai na visivyo
hai kupitia sera mbali mbali zikiwemo;
·
Haki ya Hifadhi ya Mazingira na misitu.
Rejea Qur’an
(6:38), (27:60), (16:10-13), (50:7-9), (56:63-64) na (39:62).
·
Mazingira ni amana katika kulinda uhai wetu na
wa viumbe wengine.
Rejea Qur’an
(7:10) na (16:112).
·
Sera na Mafundisho ya Mtume (s.a.w) juu ya
hifadhi ya mazingira katika kuleta ustawi wa jamii.
·
Sera ya mapinduzi ya kitabia katika kutunza na
kuhifadhi mazingira yote yanayotuzunguka.
·
Sera ya usafi na uhifadhi wa mazingira ili
kuleta ustawi wa viumbe hai.
Rejea Qur’an
(6:141) na (25:2).
4. Haki za Binaadamu kwa Ujumla (Basic Human
Rights).
Uislamu
umezingatia, kulinda na kusimamia haki za msingi za kibinaadamu bila kujali
tofauti zao. Haki hizo ni pamoja na;
·
Haki za kuishi (maisha).
Rejea Qur’an
(5:32), (6:151) na (17:33).
·
Haki ya Usalama wa Maisha.
Rejea Qur’an
(5:32).
·
Haki ya kulinda na kuheshimu hadhi na usafi wa
mwanamke.
Rejea Qur’an
(17:32) na (24:2).
·
Haki ya kupata mahitaji ya lazima ya maisha.
Rejea Qur’an
(70:24-25).
·
Haki ya Uadilifu na Usawa katika Hukumu (Righ to
justice).
Rejea Qur’an
(5:8), (49:13) na (4:135).
·
Haki ya Uhuru (kila mtu kuwa huru).
Uislamu
umezingatia kila mtu kuwa huru kifikra na kutomilikiwa kama
bidhaa ya baishara.
5. Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu.
Haki
za msingi za raia waislamu na wasiokuwa waislamu katika Dola ya Kiislamu ni
pamoja na;
·
Haki ya kuendesha maisha binafsi bila kuingiliwa
na mtu yeyote.
·
Haki na uhuru wa kutoa maoni na kuamrisha mema
na kukataza mabaya.
Rejea Qur’an
(3:104), (9:71), (9:67).
·
Haki na Uhuru katika kufuata na kuabudu dini
yeyote aipendayo mtu.
Rejea Qur’an
(2:256), (6:108), (29:46) na (16:125).
·
Haki ya Kuwashtaki Viongozi wa juu wa Dola bila
upendeleo na ubaguzi wowote.
·
Haki ya kumiliki mali au rasilimali zozote za halali
na zisizoleta madhara kwa raia na Dola kwa ujumla.
Rejea Qur’an
(2:262), (2:267) na (18:32-43).
6. Haki za Maadui Katika Vita (mateka wa
Kivita).
Uislamu
unajali, kusimamia na kulinda haki ya kila mtu hata kwa maadui waliokamatwa
katika vita (mateka) walifanyiwa haki na uadilifu kama
ifuatavyo;
·
Kuhurumiwa na kutofanyiwa ukatili wowote maadamu
wamedhibitiwa.
·
Kuwapa mahitaji yao ya lazima ya kibinaadamu na kimaisha pia.
·
Kulinda uhai na usalama wa maisha yao mpaka mwisho wa
uhasama.
·
Mateka wa kivita walikuwa na haki ya kujikomboa
kwa njia zifuatazo;
o
Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali
yeyote inayokubalika.
o
Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na
maadui.
o
Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye
manufaa kwa jamii ya waislamu.
Rejea
Qur’an (47:4).
·
Masuria na mateka wanawake walikuwa na haki ya
kulindwa na kuhifadhiwa kwa kupewa wanaume waliokwenda vitani na kuishi nao
katika maisha ya ndoa ili kupata mahitaji yao
ya msingi.
·
Haki ya kumiliki mali au uchumi ulio wa halali na
usio leta madhara yeyote katika Dola ya Kiislamu.