SABABU ZA UGONJWA WA KISUKARI
Ugonjwa
wa kisukari ni ugonjwa unaotokea pale ambapo mwili unaposhindwa kuzalisha homon
za insulin au mwili kushindwa kuzalisha homon za insulin za kutosha au mwili
kushindwa kutumia homon za insulin. Wakati mwingine hutokea pale mfumo wa kinga mwilini (immune system) unapoathiri
organ ya pancrease na kuathiri uzalishaji wa homon ya insulin.
Ugonjwa
wa kisukari husababishwa na mabo mengi yakiwepo kurithi kutoka kwenye familia,
mazingira na ufumo mbaya wa maisha (life style). Japkuwa ugonjwa wa kisukari
huweza kurithi kutoka kwa wazazi au familia lakini mfumo mbaya wa maisha
huchangia kwa kiasi kikubwa pia katika kusababisha ugojwa huu wa kisukari.
Katika post hii nitazungumzia kwa namna gani mfumo mbaya wa maisha unavyoathiri
kupatikana ugonjwa wakisukari.
- Kuzidi
uzito mwilini; kikawaida mwili unahitaji uzito maalumu kulingana na kanuni
za afya. Uzito ukiwa mkubwa sna ni tatizo na ukiwa ni mdogo sana pia ni
tatizo. Uzito kuwa mkubwa zaidi unapelekea homon ya insulin kutokuzalishwa
kiwango kinacho takiwa au mwili kushindwa kutumia insulin vizuri (insulin
resistance). Zipo njia nyingi za kupunguza uzito zikiwepo kupitia vyakula,
mazoezi au kubadilisha mfumo wa maisha. Hakikisha kuwa uzito wako upo
katika hali ya kawaida. Muone daktari akupe ushauzi kuhusu uzito wako.
- Kutokufanya
mazoezi; kikawaida mazoezi yana faida kubwa sana mwilini, zikiwemo
kuufanya mwili uwe imara. Mazoezi huweza kusaidia mifumo mbalimbali ya
mwili kufanya kazi vizuri kama vile mfumo wa chakula, mfumo wa damu na
mfumo wa afya. Mazoezi huweza kumkinga mtu na magonjwa ,mbalimbali kama
vile mafua, presha ya damu, shambulio la moyo na kisukari. Mazoezi
hupunguza mlundikano wa mafuta kwenye mwili na kusaidia kuondowa uchafu mwilini
kwa njia ya jasho. Kiafya inashauriwa mtu afanye mazoezi japo kwa wiki
asikose mara tatu. Yapo mazoezi mengi tuu na yasiyo na haja na kujiumiza
saana kama vile kuruka kamba au kukumbia jogging.
- Mpangilio
wa lishe, chakula ni muhimu kwa maisha ya kiumbe chochote, ila ulaji mbaya
pia ni tatizo kwa afya ya kiumbe pia. Mtu anatakiwa ale chakula kwa namna
ambayo haitamletea madhara katika afya yake. Mtu anatakiwa ale chakula
ambacho hakitamletea kuzidi uzito au utapia mlo au kitambi. Haya huenda
yakawa na madhara katika afya ya mtu na hatimaye kupata kisukari. Chakula
chenye mafuta mengi, sukari nyingi ama chumvi nyingi vyote sio vizuri
kutumia.
- Mazingira; wakati mwingine inatokea
mazingira watubwanayoishi yakapelekea kupata kisukari kwa mfano mashambulizi ya virusi. Kuna aina ya
virus ambao wanashambulia mwili na kufanya mwili kushindwa kusazalisha
homoni za kutosha kwa ajili ya kushibiti kiwango cha sukari ndani ya damu.
- Kutithi;
unaweza kupata ugonjwa wa kisukari kwa njia ya kurithi kutoka katika
familia. Kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya kurithiwa kwa kupitia vizazi
au kurithi rangi ya ngozi urefu au ufupi kutoka kwa wazazi vivyo hivyo
kisukari huweza kurithiwa. Haijalishi kati ya baba nani ana kisukari
lakini huenda ukakipata kwa kurithi. Pia huenda wazazi wakakwa na kisukari
na wewe ukakisosa pia.
Hitimisho
Ijapokuwa ugonjwa wa kisukari ni hatari
sana lakini kama mtu atafata masharti anaweza kuishi maisha mazuri tuu kama
watu wengine. Jambo la msingi hapa ni kufuata masharti na kuendelea kutumia
dawa za kisukari . Kufanya mazoezi na kubadilisha utaratibu wa chakula.