Dola (serikali) ya Kiislamu Madinah iliposimama na kuanza
kazi za kuongoza jamii iliandamwa na maadui wa kila aina. Mtume (s.a.w) aliweka
mikakati na mbinu madhubuti za kuilinda na kuihami serikali yake ikiwa ni
pamoja na;
i.Misafara ya Kujihami
(Patrol) na Upelelezi.
Mtume (s.a.w) aliweka watu maalum kwa ajili ya kulinda mipaka
ya Dola na kupeleleza harakati za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu.
Rejea Qur’an (4:71).
ii.Kuweka Mikataba ya
amani.
Mtume (s.a.w) aliweka mikataba ya amani na makabila ambayo
hayakusilimu yaliyopembezoni mwa Dola ya Kiislamu kama, Banu Dumra, Mudlaj,
n.k.
Rejea Qur’an (9:13-15).
iii.Kupigana vita.
Njia hii ililazimika kutumika baada ya kuzidi uonevu, dhuluma
na choko choko za wazi dhidi ya Waislamu na Uislamu.
Rejea Qur’an (2:193), (9:111) na (9:29)
iv.Sera ya wazi juu ya
wanafiki.
Mtume (s.a.w) alichukua tahadhari na hatua dhidi ya wanafiki
waliojidhihirisha wazi kutengana na ummah wa waislamu kwa kuwatenga.
Rejea Qur’an (9:73), (9:84) na (9:80).
v.Sera ya Uislamu juu
ya amani.
Mtume (s.a.w) alitekeleza na kuelekeza mafundisho ya Uislamu
juu ya kutunza na kulinda amani kama fursa na dhamana katika kueneza Uislamu.
Rejea Qur’an (8:61), (16:90), (2:84), (8:5-8).
vi.Uhusiano wa
Kiplomasia na nchi za nje.
Mtume (s.a.w) aliweka sera ya wazi juu ya uandikashaji na
utekelezaji wa mikataba mbali mbali na maadui wa Uislamu kama Aqaba,
Hudaybiyah, n.k.
Rejea Qur’an (5:8), (42:40-42), (60:8).