Jumatano, 10 Januari 2018

FAHAMU NI KWANINI TUNATAKIWA TUFANYE DUA.

Asalaamu alykum.
Sifanjema zinamstahikia Allah mola wa viumbe mfalme sikubya malipo. Katika darsa fupi la leo tutajifunza umuhimu wa kuomba duwa kwa Allah. Kama ulibahatika kusoma post zilizopita  zilizozungumzia njia ambazo duwa hujibiwa. Hebu leo tuone ulazima wa kuomba dua.

1. Dua ni ibada kama Allah anavyktuambia katima surat baqarah "nikmbeni nitakujibuni" Mtume muhammad (s.a.w) anatueleza katima sunnah kuwa duwa ni ibada katika hadithi aliyoilokea imamu Tirmidhy na akasema kuwa hadithi ni sahihi.

2.Allah anamchukia mtu asiyemuomba.
Amepokea hadithi imamu Tirmidhy kutoka kwa Abuu Hurairah Allah amuwie radhi kuwa mtume (s.a.w) amesema kuwa. " yule ambaye hamuombi Allah anamchukia" yaani mtu asiyemuomba Allah ni kwamba Allah anamchukia mtu huyo.

3.Allah anapenda kuombwa.
Amesema mtume (s.a.wa) kuwa " ...... hakika Allah mwenye kushinda na aliye tukuka anapenda kuombwa....."

4.Dua hulunguza au hukinga na mabalaa yasimpate mwenye kuomba.
Amesema mtume (s.a.w) kuwa " Hakika ya dua humkinga (mtu na mabalaa ambayo ) yanayoshuka ( yaani yanayotokea) na ambayo hayajashuka. Basi jilazimisheni na dua enyi waja wa Mwenyezi Mungu.

Hivyo kwa ufupi tunatakiwa tutumoe muda wetu vizuri. Jambo la msingi ni kuwa duwa hujibiwa hatakama hatujui kama zimejibiwa. Maana zipo nia nyingi ambazo Allah hujibu maombo. Rejea lost zetj zilizopita.