Jumapili, 7 Januari 2018

NJIA 3 AMBAZO DUA HUJIBIWA.

Asalaamu alykum warahmatuLlah wabarakaatu. Sifa njema zinamstahikia Allah mola wa ulimwengu. Sala na salamu zimwendee kipenzi cha Allah mtume Muhammad (s.a.w). Amma baada ya utangulizi huo nimekusudia kuandika kwa uchache kuhusu nia hizi ambazo duwa zetu hujibiwa.
Watu wengi wamekuwa wakipatatabu kuhusu dua zo. Wengine hukata tamaa na kujuwa kuwa hawawezi kujibiwa duwa zao katu. Lahasha usifanye hivyo. Duwa ni ibada wa mujibu wa hadithi za Mtume. Mtume katika kutuhimiza duwa amesema tumuombe Allah hata chumvi.
Huwenda mtu akawa duwa yake imejibiwa lakini asijuwe kama imejibiwa. Vili duwa hujibiwa? Allah sikuzote hututakia kheri anajibj duwa zetu katika namna iliyo bora zaidi. Hebu tuone njia ambazo duwa hujibiwa.
1.Duwa huweza kujibiwa kwa kupewa kitu kilekile mtu alichoomba. Kwa mfano ukiomba pesa utapewa pesa. Majibu haya japo wakati mwingine huchelewa na wakati mwingine huwahi na pia wakati mwi gine ni ya papo kwa papp.
2.Duw hujibiwa kwa kusamehewa madhambi. Hutokea wakatk mwingine muombaji duwa asipewe kile anachotaka ila atajibiwa duwa yake kwa kusamehewa maxhambi. Hili ni bora zIdi.
Duwa pia huweza kujibiwa kwa kuandaliwa pepo au makazi ya peponi. Hapa tofauti y a hapa ni kuwa  badal ya muombaji kupewa kile anachotaka atapata nafazi ya  peponi.
Hitimisho.
Ni matuaini yangu nimeeleweka. Nawashauri waislamu waendelee kumuomba Allah kwani hauwszi juwa ni njia gani maombi yako yatajibiwa.


                  POST MUHIMU
LIjuwe dhambi kubwa kuloko yote na madhara yake.