RANGI ZA MATUNDA NA MAANA YAKE.
Unaweza kujiuliza ni kwa nini matunda yana rangi mbalimbali? Hili swali Mwenyezi mungu aliyeumba kila kitu ndiye anajuwa saidi. Ila kwa ufupi utambuwe kuwa rangi katika matunda ni dalili ya ishara flani. Katika post hii tutaona baadhi ya rangi katika matunda. Mwisho wa post hii utaweza kutambua nini kimo katika tunda utakaloliona kwa kuangalia rang.
1.rangi nyekundu
Rangi nyekundu kwenye matunda hutokana na nyembenchembe ziitwazo lycopene. Hizi ni antoxidant ambazo husaidia katika kulinda mwili dhidi ya sumu za vyakula. Sumu hizi mara nyingi huweza kuharibu seli ndani ya miili yetu. Pia sumu hizi husababisha mtu kuzeeka haraka. Chembechembe hizi pia husaidia katika kuzuia uharibifu wa seli mwilini. Huimarisha mfumo mzima wa kinga mwilini. Na pia husaidi akatika kulinda au kupunguza adhari za magonjwa ya moyo na saratani.matunda yenye rangi hii ni pamoja na tomato, matikiti, pilipili n.k
2.rangi ya njano.
Rangi ya njano kwenye matunda husababishwa na chembechembe ziitwazo beta-carotene, hizi pia ni antoxidant. Chembechembe hizi husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini. Mwili huweza kubadili beta-carotene, kuwa vitamini A. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimu sana katika afya ya mtu. Kupamabana mna maradhi mablimbali nna kuimarisha afya ya macho. Kupambana na wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo. Huimarisha afya ya ngizi na maeneo mengune yenye utando laini.miongoni mwa matunda yenye rangi hii ni viazi, karoti, maembe n.k
3.rangi ya kijani.
Rangi ya kijani husaidia kutambuwa uwepe wa vitamini Ana C. Kama inavyotambulika mboga za majani zina rangi hii. Vitamini A na C huweza kupatikana kwa wingi kwenye rangi hii. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimi katika kudhibiti mfumo mzima wa kinga mwilini. Upungufu wowote wa vitamini hivi viwili uanaweza kusababisha madhara makubwa mwilini.
4.rangi ya bluu na violet
Rangi hii hutambulisha uwepo wa anthocyanin ambayo ni antioxidat. Itambulike kuwa antioxidant zina uwezo mkubwa wa kupambana na sumu mbalimbali ndani ya mwili. Sumu hizi zinasababishwa ba vyakula tunavyokula kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivi vyenye rangi hii huwa vina vitamini C kwa kiasi kikubwa. Pia vyakula hivi vina kambakamba ambazo ni muhimu sana katika afya ya mtu.