WANITUPA
Sina changu, ndio mana,
Ulimwengu, wanibana,
Ndugu zangu, wanikana,
Wanitupa, kisa mali,
Ulimwengu, wanibana,
Ndugu zangu, wanikana,
Wanitupa, kisa mali,
Hizi pingu, zanibana,
Sina fungu, kwa watwana,
Lipo langu, kusonona,
Nipo kapa, jumba hili,
Sina fungu, kwa watwana,
Lipo langu, kusonona,
Nipo kapa, jumba hili,
Zungu zungu, naliona,
Pishi yangu, watafuna,
Kimajungu, waninena,
Huu hapa, ukatili,
Pishi yangu, watafuna,
Kimajungu, waninena,
Huu hapa, ukatili,
Cheko langu, kinipona,
Kama wingu, wanatuna,
Sumu kwangu, yakifana,
Watanipa, ya ajali,
Kama wingu, wanatuna,
Sumu kwangu, yakifana,
Watanipa, ya ajali,
Hapo tangu, lin'gan'gana,
Dhana zangu, taja pona,
Mungu wagu, bado mbona?
Tapa tapa, kweli kweli,
Dhana zangu, taja pona,
Mungu wagu, bado mbona?
Tapa tapa, kweli kweli,
Ndoto zangu, zenda kona,
Malimwengu, yanichana,
Niko pungu, yote sina,
Niko hapa, mja tuli,
Malimwengu, yanichana,
Niko pungu, yote sina,
Niko hapa, mja tuli,
Mtunzi:HD.Hassan
@SUKARI YA MASHAIRI@
Wete. Pemba
4/9/2018
02:31 asubuhi,
@SUKARI YA MASHAIRI@
Wete. Pemba
4/9/2018
02:31 asubuhi,