Jumapili, 18 Agosti 2019

MAAJABU YA TEMBO

Mwandishi: Rajabu Athuman
Phone:     bofya hapa

5.SAFARI YA DAMU KWA KILA SIKU.
Damu ni tishu iliyopo katika hali ya kimiminika. Bila ya damu mwanadamu hawezi kuishi. Moyo ndio kiungo kikuu wenye mwili chenye kazi ya kuisambaza damu mwili mzima. Ukubwa wa kiungo hichi hufanana na ngumi. Moyo husafirisha damu kwenye mishipa inayokadiriwa kuwa na urefu wa kilomita elfu tisini na saba (97) na hii hufanyika ndani ya sekunde 20 tu.



Damu imeundwa kwa seli hai nyekundu za damu, seli hai nyeupe za damu, plasma, maji na seli sahani. Kila moja kati ya hizi ina kazi yake maalumu. Katika makala hii fupi tutaona vitu hivi kwa ufupi tu. Pia itambulike kuwa kuna viumbe hawana damu kama minyoo na baadhi ya samaki. Na hii ni kutokana na jinsi maumbile yao yalivyo. Asilimia 7% ya mwili wa binadamu ni damu na mtu mzima ana damu kuanzia lita 3.7 mapaka lita 5.6.

Seli nyekunsu za damu (red blood cell), hizi kitaalamu huitwa erythrocytes na hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa yaani bone marrow. Kwa wastani seli hizi zinaweza kuishi kwa muda wa siku 120 tu baada ya kutengenezwa. Asilimia 40@ ya damu ni seli hizi na ndio ambazo zinaipa damu rangi nyekundu. Seli zina protini na haemoglobin (chembechembe nyekundu) na hizi ndio huipa rangi nyekundu. Kazi ya seli hizi ni kubeba heya ya oxygeni kutoka kwenye mapafu na kuipeleka kwenye moyo ili isambazwe zaidi mwilini. Ka kutoa hewa ya kabondaioksaidi kutoka kwenye moyo na kuipelekwa kwenye mapafu ili itolewe nje. Pia hubeba viinilishe (nutrients) kupeleka sehemu zingine za mwili.

Seli n yeupe za damu (white blood cell) kwa jina la kitaalamu huit wa leukocytes. Kazi kubwa ya seli hizi ni kupambana na maambukizi na wadudu wa baya wanaoshambulia mwili. Seli hizi zinaweza kuishi kuanzia siku moja mpaka mwezi mmoja tu baada ya kutengenezwa. Pia hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa. Seli hizi zipo aina nyingi, kuna ambazo hupambana na kula bakteria na wadudu wengine wavamizi mwilini, kuna nyingine zinatoa antibodies kwa ajili ya kusaidia kupambana.

Seli sahani (platelets) kitaalamu huitwa thrombocytes pia hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa. Sinaishi siku sita tu baada ya kutengenezwa. Kazi yao kubwa ni kugandisha damu pindi kunapokuwa na jeraha. Plasma sio seli ni maji ya njano ambayo husaidia damu huogelea vizuri kupita kwenye mirija ya damu. Asilimia 90  ya plasma ni maji, ila pia ina madimi, vitamin na viinilishe (nutrients).