Jumapili, 22 Machi 2020

KAZI ZA PROTINI MWILINI

PROTINI NI NINI?
Neno Protini asili yake ni kutoka katika lugha ya kigiriki  ”prōteios” na kwa kiingereza protein. Neno hili limeanza kutumika karne ya 19 mnamo miaka ya 1838 na Mkemia kutoka Swedish aliyetambulika kama Jöns Jacob Berzelius. Protini ni katika viinilishe muhimu sana ndani ya miili yetu. miili yetu haina uwezo wa kuhifadhi protini hivyo endapo itakuwa nyingi itabadilishwa kuwa fati na kupelekwa maene mengine ya mwili.
NI ZIPI KAZI ZA PROTINI?
kazi za protini ni nyingi sana ndani ya miili yetu. ikiwemo:-
1. kujenga mwili
2. kupona kwa majeraha na vidonda
3. kutengeneza enzymes
4. kutengeneza homon
5. kutengeneza hemoglobin
6. kutengeneza antibodies

Enzymes ni vichochezi vya kichakato ya kikemikali ndani ya miili yetu. Hizi husaidia katika mmeng'enyo wa chakula. katika kukivunjavunja chakula kuwa virutubisho (nutrients) enzymes hufanya kazi kubwa maeneo hayo.


Miili yetu inahitaji homoni kuweza kufanya shughuli mbalimbali. Mfumo wa uzazi unahitaji homoni ili uweze kufanya kazi. Homoni zikisumbua kwenye mfumo wa uzazi mwanaume ama mwanamke atakuwa na matatatizo ambayo yanaweza pia kupelekea kushindwa kuzalisha ama kupata ujauzito.
Homoni ni kemikali zinazotolewa na tezi za mwili na kusafiri kupitia mfumo wa mzunguko wa damu hadi ogani za mwili. Humo zinasababisha mabadiliko katika kazi ya ogani. Kwa lugha nyingine zinapeleka ujumbe kwa ogani (Wikipedia)
Hemoglobin hizi ni chembechembe zinazopatikana kwenye damu. kazi yake ni kunasa hewa ya oksijeni kutoka kwenye mapafu na kuipeleka maeneo mengine kwa kupitia mfumo wa damu, na pia chembechembe hizi hunasa hewa chafu ya carbondioxide kutoka ndani ya mwili na kuipeleka kwenye mapafu ambapo huko ndipo itatolewa nje.

Antibodies hizi ni kamikali ambazo zinapatikana ndani ya damu. Kazi za kemikali hizi ni kuhakikisha mwili unakuwa salama dhidi ya mashambulizi ya Maradhi na magonjwa. Chembechembe hizi ni muhimu katika mfumo wa kinga mwilini.

VYAKULA VYA PROTINI
Unaweza kupata protini kwa kula vyakula kama
1. Samaki
2. Mayai
3. Maziwa
4. Nyama
5. Maharagwe na jamii yake kama kunde
6. Nafaka kama mchele
7. Mboga za majani kwa kiwango kidogo
8. Dagaa
9. Senene na kumbikumbi

Pia kuna hasara za kiafya za kula protini kupitiliza:
1. kuzidi kwa uzito
2. Urahisi wa kutengenezwa kwa seli za saratani
3. Moyo na figo zinaweza kuwa hatarini