Jumanne, 3 Machi 2020

kwanini Uislamu Umekataza Kutamani Mauti (kifo)


Mauti yanaogopesha sana, kwani ni yenye kukatisha raha za dunia kwa wale waliokuwa wakifurahia raha zao. Lakini wapo watu ambao wanafikia hatua mpaka wanatamani kufa na hii ni kutokana na maradhi, shida taabu ama uchamungu walio nao. Haijalishi vyovyote vile lakini Mtume (s.a.w) amekataza kuomba ama kutamani kifo. Iwe uwe na matatizo ama uwe ni mchamungu sana.


Katika mapokezi ya Abuu huraira kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Asitamani mmoja wenu Mautu (kifo) ima akiwa ni mwema kwani huenda akazidisha heri ama akiwa ni muovu huenda akatubia.
عنْ أبي هُريرة رضيَ اللَّهُ عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ : » لا يَتَمَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ إِمَا مُحسِناً ، فَلَعَلَّهُ يَزْدادُ ، وَإِمَّا مُسِيئاً فَلَعَلَّهُ يَسْتَعْتِبُ « متفقٌ عليه، وهذا لفظ البخاري

Hadithi hii inataja baadhi tu ya sababu ambazo zinawafanya watu hata wakatamani mauti. Hadithi hii inatufundisha kuwa
1. Mtume amekataza kutamani mauti
2. Usitamani mauti hata ukiwa na mwema au muovu
3. Uhai unaweza kukupa fursa akatubia madhambi kama ukiwa muovu
4. Uhai unaweza kukupa furasa ukaongeza kufanya heri zaidi kama utakuwa mwema.

Lakini inaweza ikatokea kuwa kwa matatizo mtu aliyonayo kama maradhi yasiyotarajiwa kupona na yenye maumivu makali. Mtu akiwa katika hali kama hii bado anatakiwa katu asitamani kufa. Ila kuna maneno ambazo Mtume (s.a.w) ametufundisha kuyasema:


وعن أنسٍ رضي اللَّه عنه قال : قالَ رسولُ اللَّه صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : لا يَتَمَنَّيَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ لِضُرٍّ أَصَابَهُ فَإِنْ آانْ لابُدَّ فاعِلاَ ، فَلْيَقُل : اللَّهُمَّ أَحْيِني ما آانَتِ الحَياةُ خَيْراً لي ، وتَوَفَّني إِذا آانَتِ الوفاةُ خَيراً لي « متفقٌ عليه
Katia hadithi iliyopokewa na Anas kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa Amesema Mtume (s.a.w) kuwa “asitamani mmojawenu mauti kutokana na madhara yaliyompata, na ikiwa hanabudi (ila ni kufa ama kutamani mauti ) basi na aseme “ALLAHUMMA AHYINII MAA KANAT ALHAYAAT KHIRAN LII, WATAWAFFANII IDHAA KAANAT ALWAFAAT KHAIRAN LII” (“Ewe Mwenyezi Mungu nipe uhai ikiwa uhai ni bora kwangu na unifishe ikiwa kifo ni bora kwangu”