Jumamosi, 28 Machi 2020

Vyakula Vy Vitamini B na Faida za ke mwilini




Vitamini B na faida zake mwilini
Vitamini B ni muhimu katika miili yetu kwani vina kazi ya kuhakikisha mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli (metabolism) kwa ajili ya kuzalisha nishati ama nguvu, kwa ajili ya kuondoa uchafu kwenye seli ama kwa ajili ya kutengeneza asidi mbalimbali. Kwa hakika miili yetu inahitaji vitamini B kwa ajili ya afya ya ubongo, ngozi, mfumo wa fahamu, mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na hata utengenezwaji wa seli mpya mwilini. Katika makala hii nitakwenda kukueleza kwa ufupi, kuhusu vitamini B chanzo chake, kazi zake, upungufu wake na makundi yake.


Kazi za Vitamini B mwilini kulingana na makundi yake.
Vitamini B vipo katika makundi mengi yakiwemo B1, B2, B3, B5, B6, B7, B9, B12. kila moja kati ya hivi huwa na faida yake. Kwa mfano. B1 husaidia katika ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu hususani katika neva, B2 husaidia katika uzalishwaji wa nishati na utengenezwaji wa antioxidant, B3 husaidia katika metabolism kwenye seli, B6 husaidia katika utengenezwaji wa hemoglobin pia kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu, B9 husaidia katika kuchakara DNA na kukomaa kwa seli, na B12 husaidia katika uengenezwaji wa seli mpya.


  1. Mayai
  2. Maziwa
  3. Mimea jamii ya maharagwe ama kunde
  4. Nafaka kama mchele, mahindi na mtama
  5. Alizeti na mimea jamii hiyo
  6. Mboga za majani jamii ya spinachi
  7. Mtunda kama palachichi na ndizi
  8. Viazi

1. Kupata ugonjwa wa naemia (upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini)
2. Misuli kupoteza ujazo wake
3. Kutokea kwa vidonda kwenye mdomo ama kupasuka kwa mmdomo
4. Hasira za mara kwa mara
5. Kuharisha
6. Kusahausahau

Athari za upungufu wa vitamini b mwilini
1. Kutokuona vyema
2. Kutapika
3. Kuwa na kiu kikali
4. Kupata kichefuchefu
5. Upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini kutokana na ugonjwa wa anaemia

Makala nyingine kwa ajili yako: