KUKAFINI MAITI
Imetayarishwa Na: Abu ‘Abdillaah
Yampasa kumkafini maiti na vile vile yapasa gharama za sanda zitokane na mali
ya maiti mwenyewe kama alivyosema Mtumeوسلم وآله عليه اهلل صلى wakati alipofariki
mtu akiwa katika hali ya kuhirimia, “Mkafinini kwa nguo yake” [Al-Bukhaariy na
Muslim]yaani vazi lake la ihraam na huko kumkafini (kumpamba) maiti
kunatangulizwa kabla ya deni lake kulipwa kama analo na hata kabla ya
kuutekeleza wasiya wake wa Mirathi.
Sanda huwa ni shuka tatu (3) tu, na si zaidi, kutokana na Hadiyth iliyosimuliwa
صلى اهلل عليه وآله Mtume Alikafiniwa:“رضي هللا عنها Aaishah ‘Waumini wa Mama na
وسلم katika nguo tatu nyeupe, hakuna kanzu wala kilemba katika sanda
hizo.” [Imaam Ahmad na Abu Daawuud]. Hili la sanda vipande vitatu ni kwa
wanaume na kwa wanawake kwani Hadiyth hapo juu inaweka kanuni ya jumla
na hakuna kauli iliyokuja kutofautisha baina yao. Ama Hadiyth inayoeleza kuwa
mwanamke anakafiniwa kwa vipande tano, hiyo ni Dhaifu.
Ni wajibu kumvika sanda nzuri maiti, au thamani ya sanda itokane na mali ya
maiti, ndugu zake, jamaa zake, na isiwe sanda ya thamani kubwa, na avikwe
maiti sanda hiyo kwa utaratibu alofundisha Mtume وسلم وآله عليه اهلل صلى bila kuzidisha
chochote, na amesema Mtume وسلم وآله عليه اهلل صلى” Mmoja wenu anapomvika sanda
ndugu yake, basi amvike sanda iliyo nzuri akiweza.” [Muslim, Abu Daawuud, na
Ahmad]. Na makusudio ya sanda nzuri ni ile sanda ilio safi na yenye kutosha
kumsitiri maiti mwili wake wote, na sio kufanya israfu katika sanda kwa
kununua sanda ya thamani kubwa kama alivyofafanua Imaam ‘Abdullaah bin
Mubaarak.
Endapo maiti huyo hakuwa na uwezo wa kuwa na sanda basi jamaa zake wenye
kuhusiana naye watakuwa na wajibu wa kuandaa sanda kwa ajili yake. Nao ni
watu wake kama baba yake, babu, mwanae wa kiume au mtoto wa mwanae
(mjukuu). Na endapo wote hao watashindwa au atakuwa hana jamaa, basi
litakuwa jukumu la ‘Baytul Maal’, yaani litatolewa fungu kutoka katika hazina ya
Waislam kama ipo, na kama haipo basi litakuwa jukumu la Muislam yeyote
aifahamuye hali ya huyo maiti.
Kinachopasa kumkafini maiti ni nguo itakayomsitiri mwili mzima.
Sanda inapendeza iwe nyeupe kwa Hadiyth isemayo: “Vaeni nguo nyeupe kwani
ni vazi bora katika mavazi yenu, na mkafiniane kwazo” [Abu Daawuud, AtTirmidhiy,
na Ibn Maajah kaisahihisha].
Vipande hivyo vya sanda hutiwa harufu nzuri ya aina ya ubani uliosagwa, kisha
hukunjwa moja juu ya nyingine na pia hutiwa kwenye sanda hiyo ‘Hanuut’ aina
ya unga wenye harufu nzuri ambayo ni maalum kwa maiti na kisha baada ya
hapo maiti hulazwa juu ya hiyo sanda iliyotiwa vitu hivyo, na hulazwa chale.
Ukubwa wa shuka hizo za sanda unatakiwa uzidi kimo cha maiti kutegemea na
urefu na upana wa maiti. Kuongezwe futi mbili kuzidi kile kimo cha maiti, kwa
mfano kama maiti ana urefu wa futi sita, basi urefu wa shuka uwe futi nane na
upana uwe futi sita ili stara iwe nzuri zaidi.
Baada ya kutandikwa sanda, maiti atalazwa juu yake akiwa amefunikwa
sehemu zake za siri; juu ya kitovu hadi chini ya magoti yake. Itachukuliwa ncha
ya upande wa kulia na iletwe hadi kifuani mwake, na ncha ya kushoto itafanywa
hivyo hivyo, akishafunikwa na sanda hizo wakati huo huo itachomolewa ile
shuka au taulo aliyokuwa amesitiriwa nayo sehemu zake za siri. Utaratibu huo
utafuatwa kwa shuka ya pili na ya tatu. Kisha sanda hiyo husokotwa mwisho
wake na kuanza kufungwa ili isije ikaachia sehemu yeyote na kulegea;
husokotwa ncha ya hivyo vipande vya sanda upande wa kichwani na miguuni na
kufungwa kwa kamba zilizotayarishwa. Na hufungwa nchani na katikati ya mwili
hizo kamba kuweka himaya tu sanda zisiachie na kufunuka maiti, bila kukazwa
kamba hizo. Na anawezwa maiti kufungwa mafundo matatu hadi saba kulingana
na uimara na mahitajio.
Mpaka hapa, maiti itakuwa tayari kwa ajili ya kutekelezewa jambo la tatu
ambalo ni kuswaliwa.
Maiti ikishafikishwa kaburini na kuingizwa kwenye mwanandani, zinaweza
kamba hizo kufunguliwa au kuachwa hakuna neno.
Kukikosekana vitambaa kama ilivyotajwa juu, huruhusiwa kumkafini maiti kwa
vazi la kawaida kama shuka ya chini (kikoi) na nguo ya juu kama kanzu au shati
ila ni bora zaidi kutumia mfumo uliotajwa mbeleni.
Na kukikosekana kabisa sanda atakafiniwa kwa vazi lake alilonalo au vazi lolote
la kuweza kumsitiri, na ikiwa kakosa cha kumsitiri mfano yuko jangwani au
porini, basi atasitiriwa na kitakachopatikana kama majani, matawi au chochote
cha stara.
Mwanamke anakafiniwa kwa nguo au vitambaa vitatu kama tulivyotangulia
kutaja huko nyuma, na hakuna dalili inayothibitisha kuwa anakafiniwa kwa
vipande vitano kama baadhi ya mapokezi dhaifu yanavyoonyesha. Kuna
wanaosema kuwa mwanamke anakafiniwa kwa vipande vitano. Nao
wanategemea Hadiyth ya Layla bint Qaaif Ath-Thaqafiy inayoeleza kuwa sanda
ya kike ni nguo tano zikiwa shuka ‘Izaar’mbili, kikoi, kanzu ‘Qamiys’, na
kilemba, ‘Khimaar’. Hadiyth hii upokezi (isnadi) yake ni dhaifu. Ndani ya
msururu wa wapokezi (isnadi) kuna mtu mmoja, anaitwa Nuuh bin Haakim AthThaqafiy,
ambaye hajulikani zaidi ya jina lake tu, kama alivyoelezea al-Haafidh
bin Hajar na wengineo. Hivyo itabaki kuwa mwanamke hukafiniwa kama
mwanaume kwa vipande vitatu maadam hakuna dalili sahihi ya kutofautisha
mwanaume na mwanamke katika kafan.
YASIYOFAA
Kutumia zaidi ya sanda tatu.
Kutumia sanda za ghali.
Kuandika jina la maiti kwenye kikaratasi au maneno mbalimbali kisha kukitia
ndani ya sanda azikwe nayo.
Kutumia kipande cha sanda cha ziada kuzungushia sehemu za siri za maiti.
Kuandika baadhi ya du’aa au Aayah za Qur-aan juu ya sanda.